Umoja wa Mataifa umeamua kuiorodhesha Israeli miongoni mwa nchi na mashirika yenye kudhuru watoto katika maeneo ya migogoro.
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amemuarifu muambata wa jeshi la Israeli mjini Washington Meja Jenerali Hedi Silberman kuhusu uamuzi huo, imeripoti Israel National News.
Guterres ameripotiwa akisema Israeli itawekwa katika orodha hiyo.
"Kuingizwa kwa Israeli katika orodha hiyo ni tatizo kubwa sana na inaweza kusababisha nchi kuiwekea vikwazo vya silaha Israeli,” kimesema chombo hicho cha habari, na kutaja chanzo chenye ufahamu wa taarifa hiyo.
TRT World