Mpox, ambayo hapo awali ilijulikana kama 'Monkeypox, inaweza kutibiwa kupitia chanjo. /Picha: Reuters

Takriban miezi mitatu baada ya maambukizi ya hapo awali kuripotiwa nchini. Maelezo kutoka kwa wizara hiyo yanaonyesha kifo hicho kiliripotiwa Masindi kutoka kwa mtu anayeugua na virusi vya ukimwi.

Kulingana na ripoti iliyonukuliwa kutoka kwa Wizara ya Afya na vyombo vya habari nchini Uganda, Wilaya ya Masindi imesajili maambukizi matatu ya ugonjwa wa Mpox, ambao hutambulika kwa kutoka majipu yaliyojaa usaha usoni, sehemu za siri na sehemu zingine za mwili.

Akizungumza na maofisa wa afya na viongozi wa wilaya wakati wa Misheni ya Kudhibiti Mpango wa Pamoja wa Afya wa Mwaka jijini Kampala siku ya Jumatano, Dkt. Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya, alitoa wito wa kuanzishwa upya kwa vikundi maalum vya kupambana na Mpox, kama vile ilivyokuwa wakati wa Covid-19.

Mlipuko wa Mpox, tunaweza kudhani ni suala rahisi lakini hali halisia ni suala gumu. Mlipuko huu ambao umeathiri dunia nzima unahitaji kudhibitiwa na kukomeshwa.

Nchini Uganda, maambukizi haya yalithibitishwa tarehe 24 Julai, 2024," alisema.

"Mlipuko unaendelea kuenea. Hadi sasa, tuna jumla ya maambukizi 153, kati ya hizo 42 zilikuwa katika wiki moja iliyopita. Katika siku chache zilizopita, idadi ya maambukizi inaongezeka kwa kasi," aliongeza.

Dkt. Aceng alifichua kuwa wilaya 19 zimeripoti maambukizi. Ilioathirika zaidi ni Kampala yenye maambukizi 55, ikifuatiwa na Nakasongola, jumuiya ya wavuvi, ambayo ina maambukizi 35, na Wakiso yenye maambukizi 23.

"Tulipoteza mtu mmoja, ambaye alikuwa anaugua ukimwi, mwenye CD4 kiwangi cha chini sana. Na hii inasisitiza kwamba watu ambao hawana kinga, na watoto wako hatarini kuambukizwa na virusi vya Mpox. Watu wanaoishi na ukimwi ambao hawatumii dawa zao vizuri na kutokuwa na udhibiti mzuri wa virusi wako hatarini," alisema.

Eneo la mji mkuu wa Kampala (Kampala na Wakiso) linaloongoza kwa maambukizi kama ilivyokuwa wakati wa Covid-19 ambapo maambukizi mengi pia yalikuwa katika eneo hilo.

Wanasayansi walieleza kuwa miji ina hatari kubwa ya kuenea kwa magonjwa kwa sababu ya mkusanyiko mkubwa wa watu na ni vitovu vya biashara ya kimataifa na uhamaji, ambayo huongeza hatari ya kuambukizwa.

TRT Afrika