Polisi wa Uganda wanaendelea na uchunguzi na wamesema bado kuna tisho la shambulio la kigaidi nchini Uganda / Picha : AP

Polisi wa Uganda wamewakamata watu wengine watano na kugundua mabomu mengine matano karibu na mji mkuu Kampala katika njama ya kulipua bomu inayohusishwa na kundi la waasi wa Kiislamu, jeshi hilo lilisema.

Mamlaka ya Uganda ilimshikilia mshukiwa wa kwanza akiwa na bomu kwenye begi nje ya kanisa lililojaa siku ya Jumapili, na kusababisha msako ambao ulipeleka kukamatwa kwa watu wengine watano na kupatikana kwa vilipuzi vingine vitano, polisi walisema.

Kwa mujibu wa shirika la Reuters mabomu hayo yalilipuliwa kwa usalama na vitu vikiwemo misumari, betri na vifaa vya kulipua vya unga unga vilipatikana, polisi walisema katika taarifa Jumatatu jioni.

"Mazingira ya tishio bado yapo ... ambayo yanahitaji umakini wakati wao (Waganda) wanaenda madukani, kusafiri, katika maeneo ya ibada, kusherehekea na kwa vitu vyovyote vya kutiliwa shaka, shughuli zisizo za kawaida au tabia," polisi walisema.

Washukiwa hao bado hawajatangazwa kuhusika na kundi lipi, japo kumekuwepo na mashambulio ya mara kwa mara yaliyofanywa na kundi lijulikanalo kama ADF lililo na maficho yake Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

ADF imekuwa ikisema inahusika na kundi la kigaidi la Daesh.

Reuters