Chini ya uongozi wa mwananfunzi Markson Muhwezi, wanafunzi hao walisema walitaka kufikisha ujumbe wa shukrani kwa Asuman Basalirwa, Mbunge wa Manispaa ya Bugiri kwa kuwasilisha muswada huo na Spika wa Bunge kwa kuongoza vyema katika kupitisha sheria hiyo.
"Tunauita uamuzi huo kuwa ni sherehe na tunanyenyekea na kushukuru kama kizazi kipya. Umesimama kidete kwa thamani na kanuni za nchi na bara hili." alisema Muhwezi huku akimpongeza Spika wa bunge kwa kupitisha sheria hiyo.
Wakati wakipokea ujumbe wa shukrani kwa niaba ya Spika na Bunge, Asuman Basalirwa, Mbunge wa Bugiri na Mwasisi wa muswada huo, aliwapongeza wanafunzi kwa kuungana na Bunge katika kukabiliana na dunia ya Magharibi ambayo anasema inajaribu kuwazuia Waganda na ushoga.
"Tunachodai ni heshima tu, mitala ni kosa huko Ulaya lakini hatuwapi wakati mgumu kwa hilo." alisema Basalirwa akiongeza kuwa "Ninapata msisimko huu na wabunge wote na rais wa Uganda, watu walisema tulikuwa peke yetu lakini unapinga dhana hiyo mkiwepo hapa kama wanafunzi."
Basalirwa aliomba watu wote wasome na waielewe sheria kwa mapana na marefu ili wajue haina shida na inalenga kuwalinda vijana na wazee wote.
Rais wa Uganda amesaini sheria inayopinga ushoga inayoungwa mkono na wengi katika nchi hii ya Afrika Mashariki, lakini inalaaniwa sana na wanaharakati wa haki za binadamu na wengine nje ya nchi.