Serikali ya Uganda imelazimika kuongeza muda kwa viongozi wa serikali za mitaa na baraza la wanawake kwa miezi sita.
Kulingana na Raphael Magyezi, Waziri anayehusika na Serikali za Mitaa, uamuzi huo unatokana na kukosekana kwa fedha, kiasi cha dola milioni 13.5 kuendesha mchakato huo.
"Suala la pesa sio jukumu langu, naomba Waziri wa Fedha. Unaona kazi hii ni ya sekta nyingi. Pia inahusu Wizara ya Fedha kwa sababu wao ndio watafute fedha. Tume ya Uchaguzi haiwezi kuandaa uchaguzi kama hakuna fedha za kutekeleza jukumu hilo," amesema Magyezi.
Waziri huyo aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari, bungeni nchini Uganda na kuweka wazi kuwa hatamu ya viongozi walioko madarakani ilikuwa imefikia tamati. Kulingana na Magyezi, uamuzi wa kuwaongezea viongozi hao muda, utaliingiza taifa hilo katika mgogoro wa kiuongozi iwapo kutakuwepo na ombwe na viongozi madarakani.
Waziri huyo alisema kuwa Kanuni ya 11 ya Sheria ya Serikali za Mitaa, inamruhusu kuongeza muda wa uongozi kwa viongozi wa mitaa, huku pia ikiweka ukomo, ambapo muda wao hauwezi kuzidi siku 180, na nyongeza ya pili inalenga kuruhusu.
" Halmashauri ziendelee kufanya kazi ndani ya siku 180 kama kawaida kuepusha uzorotaji wa shughuli za ujenzi wa taifa ," alieleza.