Tanzania, Kenya na Uganda ndio wenyeji wa michuano ya CHAN TotalEnergies 2024, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limethibitisha.

Hata hivyo, CAF haijaweka wazi viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

Nchi hizo tatu, ambazo zinazopatikana ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, pia zitakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2027.

Kwa mujibu wa CAF, safari ya CHAN TotalEnergies 2024 itaanzia na michezo ya kufuzu itakayofanyika Oktoba 25 mpaka 27 mwaka 2024, ikifuatiwa na mingine itakayochezwa Novemba 1 hadi 13 mwaka 2024.

Hatua ya pili ya kufuzu itafanyika Disemba 20 hadi 22 na Disemba 27 mpaka 29, 2024 kulingana na kalenda ya CAF.

TRT Afrika