Serikali ya Kenya na upinzani wanatazamia kuanzisha mazungumzo yenye lengo la kusuluhisha mzozo mkali wa kisiasa kufuatia maandamano mabaya yaliyofanyika sehemu tofauti nchini kutoka Machi hadi Julai .
Mazungumzo ya Jumatano yataendeshwa na kamati ya pamoja ya wanachama 10 kutoka serikali na upinzani, na yanapaswa kuanza saa tano unusu asubuhi.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameandaa maandamano ya siku 10 tangu Machi yaliyozua makabiliano makali kati ya raia na polisi .
Kati ya malalamiko ya upinzani yalikuwa kutaka ukaguzi wa uchaguzi wa mwaka jana uliomwingiza Rais William Ruto mamlakani.
Takriban watu 20 wamekufa katika maandamano hayo, kulingana na takwimu rasmi, ingawa wanaharakati wa haki za binadamu waliweka idadi kubwa zaidi ya vifo hivyo.
Maandamano hayo yalizua taharuki ndani na nje ya nchi na kuibua wito wa upatanishi.
Wakati wa mazungumzo
Lakini hakuna muda maalumu uliowekwa kwa muda wao na ajenda haswa ni swala zima la mzozo.
Muungano wa Azimio La Umoja wa Odinga ulisema unataka kujadili kuongezeka kwa gharama ya maisha pamoja na mageuzi ya uchaguzi baada ya Odinga kupoteza jaribio yake ya tano ya kuwania urais kwa Ruto, akidai alitapeliwa ushindi.
Hata hivyo rasimu ya ajenda ya awali haikujumuisha msukosuko wa kiuchumi wala msururu wa nyongeza ya ushuru ulioanzishwa mwezi Julai, na kukasirisha Wakenya wanaoteseka kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa za kimsingi kama vile mafuta na chakula.
Wakosoaji wanamshutumu Ruto kwa kutotimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Agosti 2022, alipojitangaza kuwa bingwa wa Wakenya maskini na kuahidi kuboresha hali yao ya kiuchumi.
Changamoto za kiuchumi
Kimani Ichung'wah, kiongozi wa chama cha wabunge wa Kenya Kwanza bungeni, chama cha Rais William Ruto, alisisitiza kuwa mazungumzo kuhusu mzozo wa kiuchumi hayatafanyika licha ya matakwa ya Azimio.