Museveni amesema mingi ya mikopo na vifurushi vya misaada haziongezi thamani kwa nchi / Photo: AFP

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema Benki ya Dunia na taasisi zingine za kigeni hazina uwezo wa kukatiza safari ya Uganda ya mabadiliko.

Benki ya Dunia imesimamisha maombi yoyote mapya kutoka Uganda ya mikopo kwa sababu Uganda ilipitisha sheria dhidi ya ushoga.

Museveni amesema mingi ya mikopo na vifurushi vya misaada, haziongezi thamani kwa nchi. Anasema nyingi huwa na athari ya maendeleo duni.

"Ninataka kusisitiza kwamba misaada na mikopo kutoka nje zinakaribishwa na zinaweza kutumika kama zimeundwa na wazalendo ,sio mawakala wa ukoloni mamboleo," Museveni amesema kwa taarifa aliyoandikia wananchi wake.

"Kinyume chake, mikopo hiyo na misaada, vinaweza kuwa chanzo cha upotoshaji na ukuaji uliodumaa kama unavyoweza kuona kote barani Afrika," Museveni amesema.

Ametoa mfano wa wizara ya Kilimo, sekta ya wanyama na uvuvi, ambapo dola milioni 800 zilikuwa za kukopa.

"Hiyo wizara haikuwa na maabara za uchunguzi wa kanda na vituo vya utafiti havikutengeneza mitambo vituo na hakuwa na kununua vifaa vya mashine kama vivunaji vya kuchanganyaau hata matrekta, hakuna vifaa vya umwagiliaji wakulima, hakuna vifaa vya kuongeza thamani," rais Museveni amesema.

"Hela hizo nyingi zilitumika kwenye semina, " Museveni amesema, " Kwa hiyo mingi ya mikopo, imekuwa haina nyongeza ya thamani kwenye safari ya mabadiliko."

Rais Museveni anauliza kama misaada na mikopo kutoka nje, ni chanzo cha mabadiliko ya kiuchumi, kwa nini hali ya sasa inakua mgogoro wa hata usalama na utulivu katika Afrika?

"Tazama katika Guinea-Conakry, Mali, Burkina-Faso, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati, DRC, Boko Haram ndani Nigeria, Somalia, Msumbij ,nyingi kati ya hizi nchi, zimekuwa zikipata ruzuku hizo na mikopo."

Anasema Uganda inatambua changamoto ambazo zikiondolewa , hata bila mikopo Uganda itaendela kiuchumi: wapangaji wa ukoloni mamboleo na wafisadi.

TRT Afrika