Baraza la Katiba la Senegal siku ya Ijumaa lilithibitisha ushindi wa mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye katika uchaguzi wa urais, na kufungua njia ya kuapishwa kwake kama rais wa tano wa nchi hiyo.
Mahakama ya juu iliidhinisha matokeo ya muda yaliyotangazwa Jumatano kulingana na hesabu za kura kutoka 100% ya vituo vya kupigia kura.
Faye alipata zaidi ya 54% ya kura katika uchaguzi wa urais uliocheleweshwa Jumapili iliyopita, huku mgombea wa muungano tawala Amadou Ba akipata 35%.
Anatarajiwa kuapishwa kuchukua nafasi ya Rais anayeondoka Macky Sall mnamo Aprili 2.
Reuters