Ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Bamako, nchini Mali.

Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa na abiria 85 imeteleza katika uwanja wa ndege wa Dakar, nchini Senegal, na kujeruhi watu 10, taarifa ya waziri wa uchukuzi wa nchi hiyo ilisema siku ya Alhamisi.

El Malick Ndiaye, waziri wa uchukuzi, alisema ndege ya Air Sénégal inayoendeshwa na TransAir ilikuwa inaelekea katika mji mkuu wa Mali, Bamako, Jumatano jioni ikiwa na abiria 79, marubani wawili na wahudumu wanne.

Majeruhi wanatibiwa hospitalini, wakati abiria wengine wamepumzishwa katika hoteli ya karibu.

Ndege hiyo ilihama katika sehemu yake ya kawaida kurukia katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Blaise Diagne, ilisema ripoti ya AFP ikinukuu taarifa rasmi.

Athari kwenye bawa

Mtandao wa Usalama wa Anga, ambao hufuatilia ajali za ndege, ulichapisha picha za ndege iliyoharibika kwenye mtandao wa X.

Kulingana na picha hiyo, injini moja ilionekana imeathirika.

TRT Afrika