Serikali ya Kenya  ilipendekeza kodi ya nyumba, hatua iliyoibua maandamano kutoka kwa wapinzani ambao walidai kuwa itazibana sana kaya za chini wakati wa kupanda kwa gharama za maisha./Picha: AA

Mahakama Kuu nchini Kenya, siku ya Ijumaa imesema kuwa uamuzi wa serikali wa kutoza kodi za nyumba ulikuwa wa kisheria.

Serikali ya Kenya ilipendekeza kukusanya ushuru wa asilimia 1.5 kwenda kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

"Tumeona kwamba tozo hizo hazina tatizo lolote na ni kwa mujibu wa katiba," alisema Jaji Josephine Mongare, wakati wa kutoa hukumu hiyo siku ya Jumanne.

Hasira dhidi ya ongezeko la kodi

Ushuru huo ulikuwa sehemu ya sheria ya fedha iliyopitishwa mwezi Juni mwaka jana.

Mahakama imesisitiza kuwa tozo hizo zilipitishwa bila kuwepo mfumo rasmi wa kisheria na kwamba uliwalenga baadhi ya Wakenya.

Sheria hiyo ilinuia kuimarisha mfumo wa ukusanyaji fedha za serikali huku kukiwa na mzigo mkubwa wa madeni na kushuka kwa kasi kwa thamani ya sarafu ya Kenya.

Hatua hiyo pia iliibua maandamano kutoka kwa wapinzani ambao walidai kuwa itazibana sana kaya za chini wakati wa kupanda kwa gharama za maisha.

TRT Afrika