Timu za uokoaji zilifika eneo la tukio hilo lililotokea Oktoba 22, 2024. / Picha: TRT Afrika  

Lori lililokuwa limesheheni mafuta lilipoteza muelekeo, kupinduka na kisha kulipa na kuua watu takribani 10, kulingana na AFP.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la njia ya panda, lililo katika mji wa Kigogwa, kilomita 25 kutoka mji mkuu wa Uganda, Kampala.

"Idadi ya watu walipoteza maisha hadi sasa ni 10, lakini kuna taarifa za majeruhi zaidi,"alisema Charles Lwanga, Mkuu wa Wilaya wa eneo hilo.

Kulingana na Lwanga, lori hilo lilipata hitilafu ya breki kabla ya kutokea kwa ajali hiyo.

Wizi wa mafuta

"Watu 10 waliungua kwa moto baada ya kikundi cha watu kuamua kuiba mafuta kutoka kwenye lori hilo," alisema.

Magari ya kubebea wagonjwa yalielekea katika eneo la tukio kwa lengo la kuwawahisha majeruhi hospitali.

Hata hivyo, moto huo ulidhibitiwa, ili kuepusha kusambaa kuelekea kituo cha mafuta kilichokuwa karibu.

Watu 19, walipoteza maisha baada ya lori la mafuta kugonga magari mengine na kulipuka nchini Uganda, katika tukio lililotokea Agosti 19, 2019.

TRT Afrika