Zamani kidogo usafirishaji wa dhahabu kutoka Zimbabwe mpaka Pwani ya Tanzania katika mji wa Kilwa uliokuwa ukikaliwa na waarabu ulitoa fursa kwa watu kuchangamana na kutumia lugha ambayo wote kwa pamoja wangeielewa kwa urahisi.
Lugha moja ikazaliwa, ambayo ilikuwa ikitumika na wakazi wa Pwani na wafanya biashara wa Kishona.
Kwa sasa inafahamika kama Kiswahili, lugha ambayo inazungumzwa na takribani watu milioni 250 katika nchi 13.
“Hii ni moja ya matoleo au mfano ya jinsi ambavyo lugha hii ilizaliwa na kuwa lugha ya mawasiliano katika ukanda wa Afrika mashariki. Kutokana na utafiti wangu, hiki ndio naamini haswa kwamba kilitokea,” anaeleza Juma Kibacha, Mkufunzi wa Historia katika taasisi ya Usimamizi wa Fedha, IFM, jijini Dar es salaam, Tanzania.
Kwa hakika kabisa, neno Swahili linatokana na neno la Kiarabu sawāḥilī – wingi wa kivumishi cha neno la kiarabu lenye maana ya ‘pwani’.
Lakini hii ni moja ya madai mengi ya jinsi ambavyo Kiswahili kilisambaa katika ukanda huu.
Lugha hii kwa sasa imekuwa ni ya kipekee, imejikita mizizi katika baadhi ya majiji, lugha yenye sifa za kipekee zinazotofautiana kutoka katika kanda tofauti.
Kwa mfano Nairobi, Sheng ni mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza ambapo lugha hii huenda sambamba kama kitambulisho cha vijana wa mjini.
Lingala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo ni Kiswahili ambacho baadhi ya maneno yamepindishwa kidogo. Hata Kituruki kina mchango wa baadhi ya maneno kama vile baba, (kelam) kalamu na daftari (deftar), kwa uchache.
Lakini hii ina maana gani kwa lugha ambayo ina historia pana, inazungumzwa na wengi na uwezo wa kufika mbali?
Je, kuna umuhimu wowote kiuchumi kuwa na kitu cha namna hii? Tukiachana na Jumuiya ya Afrika; Fikiria makubaliano ya biashara huru barani Afrika kwa kutumia lugha moja inayotuunganisha, Hebu fikiria ingekuwaje?
Ni kwa jinsi gani Kiswahili kimeweza kuenea katika ukanda huu kunaweza kuangaliwa katika maeneo manne; Hamahama ya wabantu, dini, asili yake ya wema na kuwa na uwezo wa kupokea maneno kutoka katika lugha nyingine bila kudhoofika.
Uhamaji wa Wabantu
Inakadiriwa kuwa asilimia 65 ya Afrika ni wabantu au wana uhusiano na Wabantu na wamechukua eneo kubwa zaidi ya bara hili kuliko makundi ya jamii nyingine. Ni muhimu pia kuelewa kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kibantu kitu ambacho kinafanya iwe rahisi lugha hii kupenya katika maeneo mengi.
“Lugha ilisafiri kutoka Afrika ya kati mpaka kusini, kusini mashariki mwa Afrika, kabla hatujawekewa mipaka mwaka 1885 kwenye mkutano wa Berlin na kuzuia hamahama ya wabantu,” Anaeleza Profesa Aldin Mutembei, mtafiti na mkurugenzi wa Kiswahili katika taasisi ya Confucius kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Dini na Biashara
Kabla ya ukoloni, kwa kiasi kikubwa biashara ilikuwa inafanyika kwa lugha ya Kiswahili , kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba baadhi ya maneno ya mashariki ya mbali yalitoholewa na kuingizwa katika lugha na baadhi ya maneno ya Kiswahili yakaingia katika lugha zao pia.
Maandishi husambaa kwa haraka zaidi kuliko maneno ya kuambizana, Dini ilihusishwa na Kiswahili kwa sababu waarabu walikuwa ni watu wa kwana kutunza maandiko ya Kiswahili.
Wamisionari na Wataalamu wa madini walikuwa na wakati mgumu kueneza Ukristu ili kuzuia kuenea kwa lugha ya Kiarabu kwa sababu walikuta imeshajiwekea mizizi kwenye lugha za Kibantu.
“Mswahili mzuri ni Muisalmu kwa sababu waarabu ni waislamu,” anaeleza Mutembei. Huu ulikuwa ni ujumbe kabla ya ujio wa wareno na wajerumani walifika na kukuta lugha hii ni tofauti na mfumo wao wa kirumi.
Kwa bahati mbaya inawezekana Wajerumani walisaidia kuunganisha Wabantu waliozungumza Kiswahili kwa kuamuru wazungumzaji wote wa Kiswahili kujifunza Kiswahili kwa mfumo wa alfabeti za kilatini. Kwa wale ambao walipinga agizo hilo waliamua kujifunza kwa mifumo yote miwili, mfumo wa Kiarabu na mfumo wa Kirumi.
“Cha kushangaza, lugha ya Kihausa ya Nigeria ikizungumzwa inasikika kama Kiswahili kuliko lugha nyingine zote za Naijeria hii ni kutokana na lugha hiyo kujishikiza na kiarabu.”
Biblia ya kwanza ya Kiswahili ni ya Kijerumani iliyoandikwa na Karl Roehl, ilipata wakati mgumu kupigiwa chapuo kwa Kiswahili kwa sababu haikuwa na misamiati yote ya Kiswahili inayoeleweka kwa sababu mwandishi aliondoa maneno yote ambayo yalionekana kuwa ni ya kiarabu.
Uwezo wa kupokea na kujumuisha maneno
Neno la Kiswahili la kuwa na staha “ustaarabu” lina maana ya “kuwa kama Mwarabu,” anafafanua Mutembei.
Hii ilileta changamoto hasa kwa wakoloni wa kale kulitumia walipokuwa wakijaribu kuwabadili wabantu waliozungumza Kiswahili ili wawe na fikra na mitazamo ya ‘mabwana’ zao wakoloni, hivyo ikawa ni rahisi kuongeza misamiati mipya kwenye lugha ya Kiswahili.
“Kusaidia” ni neno ambalo lugha ya Kiswahili inaweza kufanya vizuri zaidi ukilinganisha na lugha nyingine za Kiafrika.
Ina uwezo wa kukaribisha kila inapobidi, hivyo inafanikisha uwepo wa lugha zingine kama Sheng ya Kenya.
Mwaka 1963, tamasha la Kwanzaa lilizinduliwa nchini marekani likitokana na hamasa ya lugha ya Kiswahili kwa jina na kanuni zake kama Wamarekani weusi na uhusiano walionao na bara la Afrika, wafuasi wake wakajitengea sherehe ambayo itakuwa tofauti na zile za jamii ya kizungu.
Kiswahili hakiangamizi lugha nyingine
“Tofauti na Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na lugha nyingine kama hizo, ukuaji wa hadhi ya Kiswahili si wa kimashindano au kuzuia umuhimu au nafasi ya lugha nyingine.” Anaeleza mhadhiri zamani wa chuo cha Princeton Kwa Masomo ya Africa, Aldin Mutembei.
Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, aliunganisha makabila mbalimbali nchini Tanzania kwa kuamuru wote wazungumze lugha moja. Lakini hakushusha uthamani wa lugha nyingine zilizozungumzwa na makabila, hivyo mfumo wa shule ulitumia lugha ya Kiswahili katika kujifunza.
Marais Julius Nyerere wa Tanzania (1962–85) na Jomo Kenyatta wa Kenya (1964–78) walikiinua Kiswahili kuwa lugha ya kisiasa na kiuchumi na kiukombozi kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Lugha rasmi ya biashara kwenye jumuiya ya Afrika mashariki ni Kiswahili ikiwa ni pamoja na kuwekewa msisitizo wa kutumika katika nyaraka mbalimbali. Inatambulika na kukubalika na Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika, SADC, na imeongezwa kuwa ni lugha ya maswaliano wakati wa vikao vinavyoendelea.
Mwaka 2021 nchi ya Rwanda iliomba Tanzania iwapatie walimu wa Kiswahili ili kwenda kufundisha somo la Kiswahili katika shule zao.
“Tunahitaji lugha moja itakayotuunganisha kama Waafrika na Uafrika wetu, Kujitambua kwetu kutatokana na lugha, na lugha hiyo ni Kiswahili,” Mutembei anamnukuu Rais wa zamani wa Ghana, Kwame Nkrumah, katika mkutano wa kwanza wa Umoja wa Afrika.
“Ghana ilianza kufundisha Kiswahili kwenye taasisi zao 1964 na imekuwa na Kitengo cha Kiswahili katika Chuo kikuu cha Ghana. “Walikuwa ni wa kwanza kwa Afrika na wala hawakuwa taifa linalozungumza Kiswahili,” Mutembei anahitimisha.
Kutokana na kuanza kutambulika kwa Siku ya Kiswahili duniani, kutakuwa na Mkutano wa “Umoja wa Waafrika na Kiswahili kwa Afrika” Jijini Accra Julai 7, Inaweza kuwa ni ishara lugha hii kupanuka zaidi na kuzungumzwa na bara zima la Afrika kwa siku za hivi karibuni.