Mto Nairobi una urefu wa kilomita 45. /Picha: Rais William Ruto 

Rais William Ruto amezindua programu inayoitwa Climate WorX yenye lengo la kusafisha na kuupa thamani Mto Nairobi.

Mto huo, wenye urefu wa kilomita 45, unapatikana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

" Mradi wa Climate WorX utatoa ajira kwa zaidi ya watu 200,000 kote nchini na utasaidia sana kuhuhisha na kuhifadhi mazingira yetu," alisema Rais Ruto wakati akiwa Korogocho, sehemu ambayo mtu huo unapitia.

" Climate WorX utazingatia uwezeshwaji wa vijana na ushiriki wao kikamilifu katika kuboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na makazi ya kijamii, kujenga madaraja ya miguu na barabara ndogo ndogo, na kutengeneza huduma muhimu za kimwili na kijamii," Rais Ruto aliongeza.

Kulingana na Rais Ruto, mabadiliko ya hali ya tabia nchi ni tishio la wazi linalowakabili binadamu wote ulimwenguni, huku akisisitiza haja ya kukabiliana nazo 'uso kwa uso'.

"Ndio maana wachafuzi wa mazingira lazima wawajibishwe," alisema Rais Ruto, na kusisitiza kuwa mradi huo utazalisha zaidi ya ajira 200,000.

Pamoja na mambo mengine, mradi huo unalenga kurejesha uzuri wa asili wa mto Nairobi, kuondoa uchafuzi wa mazingira, na kuunda maeneo ya kijani ambayo yatawezesha kiuchumi jamii zinazozunguka Mto huo.

" Uchafuzi wa Mto Nairobi umechangiwa na ukosefu wa mifumo bora ya udhibiti taka, kutotekelezwa kwa kanuni za mazingira na mashirika husika na uelewa na elimu ya kutosha ya umma kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira," Shirika la kutetea mazingira la Green Peace linasema.

Mnamo tarehe Februari 22, 2023, Rais Ruto aliunda Tume ya Mto Nairobi, ikiwa ni kabambe wa kusafisha bonde la mto huo.

Tume hiyo ni sehemu ya mpango wa Rais wa kuboresha miundombinu ya jiji la bluu-kijani na kuhakikisha kwamba watu wa Nairobi wanaweza kufurahia uzuri wa asili wa mto huo.

Jukumu lake ni kutoa mwelekeo wa kimkakati, uangalizi na uratibu wa juhudi za ukarabati wa Mto ya Nairobi.

TRT Afrika