Kenya na Uganda kupatanisha mzozo kati ya Ethiopia na Somalia

Kenya na Uganda kupatanisha mzozo kati ya Ethiopia na Somalia

Majaribio kadhaa ya kusuluhisha mzozo yalishindwa kufanikiwa.
Marais hao wanakutana mjini Arusha Tanzania katika mkutano wa 24 wa viongozi wa Afrika mashariki /Picha: Reuters 

Rais wa Kenya William Ruto alisema siku ya Jumamosi yeye na Rais wa Uganda Yoweri Museveni watasaidia kupatanisha mzozo kati ya Ethiopia na Somalia, unaotishia uthabiti wa eneo hilo.

Ethiopia isiyo na bandari, ambayo ina maelfu ya wanajeshi nchini Somalia kupambana na waasi wenye mafungamano na al Qaeda, imetofautiana na serikali ya Mogadishu kuhusu mipango yake ya kujenga bandari katika eneo lililojitenga la Somaliland, ili kubadilishana na uwezekano wa kutambuliwa kwa uhuru wake.

Somaliland imejitahidi kupata kutambuliwa kimataifa licha ya kujitawala na kufurahia amani na utulivu linganishi tangu kujitangazia uhuru mwaka 1991.

Mzozo huo umeifanya Somalia kuwa karibu na Misri, ambayo imekuwa ikizozana na Ethiopia kwa miaka mingi juu ya ujenzi wa Addis Ababa wa bwawa kubwa la maji kwenye Mto Nile, na Eritrea, adui mwingine wa Ethiopia.

"Kwa sababu usalama wa Somalia... unachangia kwa kiasi kikubwa utulivu wa eneo letu, na mazingira ya wawekezaji na wafanyabiashara na wajasiriamali kustawi," aliuambia mkutano wa wanahabari.

Majaribio kadhaa ya kusuluhisha mzozo mjini Ankara, Uturuki, yalishindwa kufanikiwa.

Serikali ya Ethiopia na wasemaji wa mambo ya nje hawakujibu mara moja maombi ya maoni yao. Waziri wa mambo ya nje wa Somalia hakuweza kupatikana mara moja na Reuters.

Reuters