Kulingana na ripoti ambayo imevumbuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira , UNEP, karibu theluthi moja ya wakazi wa dunia wanakabiliwa na mawimbi ya joto kali zaidi ya siku 20 kwa mwaka.
Joto likizidi watu hukimbilia viyoyozi kwa ajili ya kujipoza, lakini sasa wataalamu wanasema kiyoyozi ni chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi.
"Lakini wakati huo huo, upoaji wa kawaida, kama vile kiyoyozi, ni kichocheo kikuu cha mabadiliko ya hali ya hewa, kinachowajibika kwa zaidi ya asilimia saba ya uzalishaji wa gesi chafu duniani," UN imesema.
"Ikiwa haitadhibitiwa ipasavyo, mahitaji ya nishati kwa ajili ya kupoeza anga yataongezeka mara tatu ifikapo mwaka wa 2050, pamoja na uzalishaji unaohusishwa."
Shirika la UN linaonya kuwa kadiri tunavyojaribu kujiweka baridi, ndivyo tunavyopasha joto sayari. Na ikiwa mwelekeo wa ukuaji wa sasa utaendelea, vifaa vya kupoeza vinawakilisha asilimia 20 ya jumla ya matumizi ya umeme leo - na inatarajiwa kuongezeka zaidi ya mara mbili ifikapo 2050.
Mifumo ya kisasa ya kupooza, kama vile viyoyozi (ACs) na kijofu au friji, hutumia kiasi kikubwa cha nishati na mara nyingi hutumia friji zinazopasha joto sayari.
Ripoti ya hivi karibuni ya UNEP inaonyesha kuwa kwa kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya nguvu ya vifaa vya kupoeza kunaweza kusababisha kwa angalau asilimia 60 ya vyanzo vya kuongeza joto duniani kufikia mwaka 2050.
"Sekta ya kupoeza lazima ikue ili kulinda kila mtu kutokana na kuongezeka kwa joto, kudumisha ubora na usalama wa chakula, kuweka chanjo kuwa thabiti na uchumi wenye tija," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP.
Andersen alizindua ripoti hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Expo City, ambapo COP28 imekuwa ikiendelea tangu Alhamisi iliyopita.
"Lakini ukuaji huu haupaswi kuja kwa gharama ya mpito wa nishati na athari kubwa zaidi ya hali ya hewa," alihimiza.
Katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi COP 28 zaidi ya nchi 60 zilitia saini kile kinachoitwa 'ahadi ya kupoeza' kwa ahadi za kupunguza athari za hali ya hewa kutoka kwa sekta ya baridi.