Jaribio la utekaji nyara wa meli ya kibiashara katika Ghuba ya Aden siku ya Jumapili inaonekana kutekelezwa na maharamia wa Kisomali wenye silaha na sio Wahouthi wa Yemeni, licha ya kurusha makombora kutoka eneo linalodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen baadaye, Pentagon ilisema Jumatatu.
"Tunaendelea kutathmini, lakini dalili za awali ni kwamba watu hawa watano ni Wasomali," alisema msemaji wa Pentagon Brigedia Jenerali Patrick Ryder.
Meli ya kivita ya Jeshi la Wanamaji la Marekani iliitikia wito wa dharura siku ya Jumapili kutoka kwa meli ya kemikali ya Central Park. Washambuliaji hao walichukuliwa kwenye meli ya kivita ya Marekani ya Mason, jeshi la Marekani lilisema, na meli ya CentralPark na wafanyakazi wake walikuwa salama.
Kumekuwa na mfululizo wa mashambulizi katika Ghuba ya Eden tangu vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas kuanza tarehe 7 Oktoba.
Central Park, meli ya mafuta inayosimamiwa na Zodiac Maritime Ltd, kampuni ya kimataifa ya usimamizi wa meli yenye makao yake makuu London inamilikiwa na familia ya Ofer ya Israel. Meli hiyo yenye bendera ya Liberia ilijengwa mwaka wa 2015 na inamilikiwa na Clumvez Shipping Inc, data ya LSEG ilionyesha.
Ryder aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani walifyatua risasi za onyo wakati washambuliaji walipokuwa wakijaribu kutoroka, lakini hakukuwa na majeruhi.
Aliongeza kuwa kulikuwa na meli tatu za kijeshi za China katika eneo hilo lakini hazikujibu. Ubalozi wa China mjini Washington haukuweza kupatikana mara moja ili kutoa maoni yake kuhusu madai hayo.
Jaribio la utekaji nyara wa meli hiyo lilifuatia tukio la Wahouthi kukamata meli ya mizigo yenye uhusiano na Israel kusini mwa Bahari Nyekundu wiki iliyopita. Kunid la Wahouti wanaaminiwa kuwa washirika wa Iran.