Timu 34 zinashiriki mashindano haya kutoka mataifa 20 , Picha : Ikulu Kenya 

Mashindano ya kimatafa ya magari yaani World Rally Championship, yameanza mjini Naivasha nchini Kenya.

Mashindano haya yatafanyika kwa siku nne kuanzia Juni 22.

Rais William Ruto amesema mashindano hayo tayari yameleta zaidi ya dola milioni 450.

Anasema haflla hiyo inavutia zaidi ya wageni 100,000, na kuunda nafasi za kazi zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 175.

" Kando na uundaji wa ajira, hafla hiyo itakuza tasnia ya utalii," rais William Ruto alisema .

Rais Ruto alisema mashindano hayo tayari yamevipa vyombo vya habari nchini matangazo yenye thamani ya dola milioni 57.

Mashindano hayo yamevutia timu 34 kutoka nchi 20.

TRT Afrika