Uchaguzi nchini DRc utafanyika tarehe 20 Disemba/ Picha ya TRT Afrika

Tarehe 20 Disemba, wapiga kura milioni 40 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watapiga kura kumchagua rais wao pamoja na wabunge, viongozi wa mkoa na nyadhifa za udiwani katika duru moja ya uchaguzi.

Wagombea wa kiti cha urais ni 22 / Picha: TRT Afrika

Mji wa Kinsasha umejaa mabango ya wagombeajia tofauti wa vyama tofauti ambao wanauza sera zao kwa wananchi wakiwaomba kura.

Baadhi ya mabango ya wagombea  nchini DRC. Picha/ TRT Afrika

Takriban watu milioni 40 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo mkuu, ikiwa wagombea wa kiti cha urais ni 22.

Tume ya uchaguzi nchini DRC inasema maandalizi yote yamekamilika kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Picha/TRT Afrika. 

Rais wa sasa wa DRC Felix Antoine Tshisekedi Tchilombo anatetea tena nafasi yake ya urais kwa muhula wa pili katika uchaguzi mkuu. Kufuatia uchaguzi wa 2018, Tshisekedi alichukua mamlaka kutoka kwa rais wa zamani Joseph Kabila.

Rais wa sasa wa DRC Felix Antoine Tshisekedi Tchilombo anatetea tena nafasi yake 

Kulingana na sheria za uchaguzi nchini DRC, mgombea yeyote atakayepata kura nyingi zaidi katika duru ya kwanza atakuwa mshindi wa kuwa rais hata kama hatapata zaidi ya 50% ya kura.

Jengo la ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi CENI, nchini DRC mjini Kinshasa. Picha/TRT Afrika. 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imesisistiza kuwa itahakikisa uchaguzi ulio na uwazi na wa haki . Hii inakuja huku upande wa upinzani tayari ulisema haina imani kwa tume hiyo ukidai kuwa serikali ya rais wa sasa Felix Tshisekedi itahakikisha matokeo yanamrudisha kwa kiti,

TRT Afrika