Jeshi la Israeli limelenga nyumba kadhaa za raia katika maeneo ya Gaza. / Picha: AA

Serikali ya Palestina Gaza inailaumu jumuia ya kimataifa kwa "muendelezo wa uhalifu wa kivita unaofanywa na Israel" Gaza, huku Israel ikianzisha mashambulizi katika eneo lililozingirwa punde tu baada ya muda wa kusitishwa kwa mapigamo kwisha.

"Jeshi la walowezi wa Israeli limeanzisha tena mauaji dhidi ya watu wa Palestina katika ukanda wa Gaza,” ofisi ya habari ya serikali Gaza imesema katika taarifa yake mapema asubuhi Ijumaa.

Jeshi la Israeli limelenga nyumba kadhaa na maeneo ya raia katika eneo la Gaza, ofisi hiyo imesema, na kusisitiza: “Jumuia ya kimataifa ina jukumu la kulaumiwa kwa muendelezo wa uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya ukanda wa Gaza.”

Wizara ya Afya Gaza imeripoti kwamba Wapalestina 32 wameuawa katika mashambulizi ya mabomu ya Israel yanayoendelea.

Ndege za kivita za Israeli zimelenga maeneo kadhaa ya Gaza mapema Ijumaa. 

“Jumuia ya kimataifa, hasa Marekani, Rais wa Marekani, Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, wanahusika na uhalifu unaofanywa na walowezi wa Israel na mauaji yao dhidi ya raia, watoto na wanawake Gaza," imeongeza.

Taarifa hiyo pia imesema: “Sheria za vita na sheria za kimataifa za kibinadamu zimekiukwa. Jumuia ya kimataifa imeipa Israel ishara ya kuendelea na mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.”

Mashambulizi kadhaa ya anga

“Watu wa Palestina wana haki ya kujitetea kwa namna yoyote, kupata uhuru wao, na kuanzisha taifa la Palestina na Jerusalem kama mji mkuu kutokana na sheria za kimataifa, na kuwaondoa kabisa wanaokalia ardhi yao,” imesema.

Ndege za Israeli za vita zimelenga maeneo kadhaa ya Gaza mapema Ijumaa, hayo ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Anadolu ambae yuko katika eneo hilo.

Vikosi vya uokozi vya Palestina na wananchi wamekusanyika kutafuta na kuokoa katika kifusi cha nyumba kufuatia mwisho wa wiki ya usitishaji wa mapigano baada ya shambulizi la Israel katika kambi ya Al Maghazi.

Kusitishwa kwa mapigano kati ya Israeli na Hamasi, ambayo yalianza Novemba 24, kumeisha asubuhi Ijumaa.

TRT World