Imam Hassan Sharif alipigwa risasi baada ya saa kumi na mbili za asubuhi nje ya msikiti wa Masjid-Muhammad-Newark, maafisa wanasema. / Picha: Masjid-Muhammad-Newark

Imamu wa msikiti amepigwa risasi nje ya msikiti wa Newark katika jimbo la New Jersey amefariki kutoka na majeraha ya risasi, mamlaka nchini Marekani imesema.

Mwanasheria wa New Jersey Matt Platkin amesema siku ya Jumatano kuwa kifo cha Imam Hassan Sharif unaombolezwa jimbo zima, na kuongeza kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa mauaji hayo yalikuwa na mrengo wa dini.

Kiongozi huyo wa dini ya Kiislamu alikuwa katika gari yake pindi alipopigwa risasi zaidi ya mara moja karibu na msikiti, mwendesha mashtaka wa kaunti ya Essex Ted Stephens amewaambia waandishi wa habari.

TRT World