Uturuki imesema kwamba Israel kukata kwa njia zote za mawasiliano, kuna lengo la kuzuia mawasiliano yote ya kimataifa yanayounganisha Gaza na dunia ya nje "ni ishara tosha ya nia ya kufanya uhalifu wa kivita."
"Hizi ni jitihada za kuficha ukweli wa uharibifu wa Israel kwa maisha ya raia," Fahrettin Altun, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki amesema siku ya Ijumaa baada ya Israel kutangaza kufanya "uvamizi" wa ardhini ndani ya Gaza iliyozingirwa.
Israel kwa mara nyengine, inaonyesha kwamba haina dhamira ya kulinda raia au kuheshimu misingi ya haki za binadamu, Altun alisema katika mtandao wa X, ambao zamani ulikuwa Twitter.
"Kukata kabisa mawasiliano ya simu za mezani, mkononi, na mawasiliano ya mitandao Gaza, kunaashiria hatua ya mwisho ya jeshi la Israel dhidi ya watu wa Palestine."
Afisa huyo wa Uturuki amesema huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi yake dhidi ya eneo dogo la Palestine, hatua yake ya kuharibu miundombinu ya mawasiliano ni shambulizi la wazi dhidi ya misingi ya kibinadamu. "Pia ameshutumu nchi za Magharibi kwa kuendelea kushindwa kuchukua hatua "katika uhalifu huu ambao unawafanya nao wawe sehemu ya uhalifu."
"Kutojali ubinadamu kwa watu wa Gaza na adhabu jumuishi inayowalenga wote haina uhalisia wa kujitetea." Altun amesema wale wanaopinga uwezo wa Israel wa kufanya mashambulizi kwa wote bila kujali matokeo "lazima wajiangalie tena waliposimama."
"Ni sharti wajue kwamba msimamo wao wa kutochukua hatua katika masiku haya mabaya kabisa utakuwa na doa la maisha katika historia yao."
Akiitisha usitishwaji wa haraka wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, Altun amesema mataifa yenye nguvu duniani yanayounga mkono uhalifu wa Israel kwa Palestine "hawana haki ya kumfundisha mtu yoyote maadili kuanzia sasa na kuendelea."