Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu Rwanda kwa madai ya kuliunga mkono kundi hilo, licha ya madai hayi kupingwa na Rwanda./Picha: Reuters

Mji wa Kalembe, ulio katika eneo la kijeshi la Kivu Kaskazini, limekuwa chini ya himaya ya M23 siku ya Jumapili asubuhi baada ya waasi hao kuutwaa kutoka Jeshi la DRC.

Kikundi cha M23 kimekuwa kikisababisha machafuko katika nchi hiyo kutoka mwaka 2022.

Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu Rwanda kwa madai ya kuliunga mkono kundi hilo, licha ya madai hayi kupingwa na Rwanda.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa Jeshi la DRC, Sylvain Ekenge alithibitisha kukombolewa kwa mji Kalembe. Hata hivyo, kiongozi wa Congo River Alliance (AFC) Corneille Nangaa, amesema kuwa bado M23 walikuwa wanashikilia eneo hilo.

Kulingana na Ekenge, mapigano kati ya wanamgambo wa serikali na M23 yalikuwa yakiendelea.

Vikosi vya kijeshi vilisafirishwa kwa njia ya helikopta siku ya Jumatatu, kukabiliana na hali hiyo, alisema.

Afisa mmoja kutoka eneo la Walikale, Kabaki Alimasi, amethibitisha jeshi kutwaa eneo hilo, huku akisema mapigano yalikuwa yakiendelea karibu na eneo hilo.

TRT Afrika