Jeshi la Anga la Uganda lilishambulia makao manne ya kundi la ADF / Picha: AFP

Serikali ya Uganda imesema kuwa Meddie Nkalubo ambae anadaiwa kuhusika katika mashambulizi yaliyotokea katika Kituo cha Polisi Cha Kawempe, karibu na Bunge la nchi hiyo, na mashambulizi ya kujitoa muhanga karibu na kituo cha basi cha Swiftbus.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ametangaza Jumamosi kuwa Jeshi la Anga la Uganda lilivamia makao manne ya kundi la ADF yaliyokuwa kati ya kilomita 100 na kilomita 150 kutoka mpaka wa Uganda na DRC, Ntoroko na kuwauwa wanachama wa kundi la ADF.

"Kulingana na taarifa za kijasusi, magaidi wengi waliuawa, pamoja na mpiganaji sugu Meddie Nkalubo ambaye amekuwa mratibu wa mashambulio ya mabomu jijini Kampala na kuhusika kwenye matukio kama Kituo cha Polisi huko Kampala, tukio la karibu na Bunge na yale yaliyotokea hivi karibuni karibu na Kanisa la Kayanja na katika eneo la Bunamwaya," Museveni aliandika kwenye mtandao wa X.

Wazazi waliokuwa na majonzi baada ya ADF kuvamia shule ya Lhubiriha mashariki mwa Uganda. Picha ADF

Aidha, rais Museveni ametoa shukrani kwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kwa kuiwezesha Uganda kutekeleza operesheni hiyo.

"Tunampigia saluti rais Felix Tshisekedi kwa kuturuhusu kufanya kazi na Jeshi la Kongo ili kuikomboa sehemu hii ya Kongo kutoka kwa wahalifu hawa wasio na akili, " Museveni aliongeza.

Museveni amesema kuwa Uganda bado ina uchungu wa mauaji ya hivi karibuni dhidi ya raia wake na kuwa wahusika hao 'watagundua kuwa kuwaua Waganda sio jambo zuri.'

"Wote waliohusika katika mauaji ya hivi karibuni ya watoto wa Nyabugaando kwa kuwakata na mapanga masheikh, meja Kiggundu, binti yake jenerali Katumba, Joan Kagezi, nk. wataangamia hadi wajisalimishe," alimaliza.

Katika upande huu wa Ulimwengu, hakuna mahali ambapo hatuwezi kuwapata, ikiwa tutaratibu na Serikali za nchi njirani na pia kuwaadhibu kwa kuwaua Waganda kwa kutumia waingiliaji.

Rais Museveni

Kundi la ADF linadaiwa kuwaua watu wapatao 4,000 nchini Kongo na wengine nchini Uganda. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Mradi wa Takwimu za Eneo la Tukio la Migogoro ya Silaha, kinachofuatilia makanisa, migahawa na maeneo mengine ya raia.

TRT Afrika