Polisi nchini Kenya wamefukua miili 12 zaidi inapoendela na uchunguzi dhidi ya kikundi kinachodaiwa kufanya ibada ya njaa katika msitu wa Shakahola, pwani ya Kenya.
''Idadi ya waliofariki imefika 372,'' Kamishna wa Polisi wa Mkoa Rhoda Onyancha alitangaza Jumatano.
Ufukuaji huo ulifanyika katika siku ya tatu ya awamu ya nne ya operesheni hiyo.
Polisi walisema kupatikana kwa miili hiyo kunaashiria hatua nyingine mbaya katika uchunguzi wa shughuli za ibada hiyo, ambayo imevutia umakini mkubwa katika miezi ya hivi karibuni.
“Tumeshika doria na kuwasaidia wapelelezi wa mauaji kupekua msituni, na tumegundua makaburi kadhaa. Ni lazima izingatiwe kuwa ni msitu mkubwa, ambao unafanya oparesheni iwe polepole na ngumu,” vyombo vya habari vya ndani vinamnukuu Onyancha akisema.
Mamlaka zinasema kuwa zimekuwa zikifanya kazi kwa bidii kuwaokoa watu waliokuwa chini ya udhibiti wa kanisa hilo.
Onyancha alisema kuwa tangu Aprili, watu 95 wameokolewa kutoka kwa kanisa hilo, linaloongozwa na mchungaji Paul Mackenzie.
Viungo vilivyopotea
Watu hawa, ambao walivumilia uzoefu wa kutisha, sasa wanapokea usaidizi unaohitajika na utunzaji ili kuwasaidia kujumuika tena katika jamii.
Ilikuja siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kithure Kindiki kusema kwamba maafisa wa usalama walioruhusu ibada hiyo kufanya kazi watakabiliwa na sheria
Alisema mamlaka imefukua makaburi mapya 40 ya pamoja.
Mamia ya maiti zimepatikana katika msitu wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi tangu Aprili wakati wa uchunguzi kuhusu dhehebu hilo linaloendeshwa na Mackenzie, anayeongoza Kanisa la Good News International nchini Kenya.
Anashtakiwa kwa kuamuru wafuasi wake kujizuia kula au kunywa hadi wafe ili waweze kwenda mbinguni.
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya viungo vya waliathiriwa vilikosekana, jambo ambalo limesababisha dhana kuwa huenda alikuwa akifanya kazi ya kusafirisha viungo vya binadamu.