Kenyans seek relatives among starvation cult victims in Kilifi / Photo: Reuters

Maiti hizo zilizokutwa zimezikwa katika msitu wa Shakahola karibu na mji wa pwani wa Malindi ulisababisha mshtuko miongoni mwa Wakenya, huku kiongozi wa waumini hao Paul Mackenzie Nthenge akishutumiwa kuwasababishia wafuasi wake kifo kwa kuhubiri kuwa kukaa njaa ndio njia rahisi ya kufika mbinguni.

"Tulikuwa na changamoto nyingi leo kwa ajili ya mvua, lakini hatimaye tuliweza kufukua maiti nane,” polisi walielezea shirika la habari la AFP, ambapo sasa jumla ya maiti zilizo fukuliwa zimefikia 98. "tutaendelea na oparesheni hii’’ waliongezea kusema.

Kisa hicho cha ajabu ambachoi kimepewa jina "mauaji ya halaiki ya Shakaola” kimesababisha kutolewa wito wa kuanzisha msako dhidi ya makanisa bandia, katika nchi hiyo inayoaminiwa kuwa na wakristu wengi.

"[Nthenge] Aliwaagiza wajinyime kula na kunywa kujiandaa kwa mwisho wa dunia wa tarehe 15 Aprili na kuwa yeye ndiye atakaye kuwa wa mwisho kufunga milango na kuondoka” alisim,ulia Steven Mwiti, ambaye mkewe na wanawe walijiunga na knaisa hilo na wanaaminiwa kuwa miongoni mwa waliokufa.

Mwiti anasema kuwa alipata habari hii kutoka kwa mmoja wa waumini wa kanisa hilo ambaye alifukuzwa baada ya kukiuka amri ya kutokunywa maji wakati wa mfungo huo wa kujiua.

Hospitali kadhaa katika mji huo wa pwani wa Malindi, ambazo zimekuwa zikiwapokea manusura pamoja na maiti, zinasema kuwa wamesikia maelezo kama hayo kutok akwa manusura.

Kenyans seek relatives among starvation cult victims in Kilifi

"[Nthenge] alikuwa na mpango bayana wa kuwaua mwanzo watoto, vijana kisha watu wazima, halafu yeye atakuwa wa mwisho kujiua” alisema mmoja wa wafanyakazi wa hospitali aliyetaka tulifiche jina lake.

Mwiti anasema alipiga ripoti katika kituo cha polisi lakini anahisi kuwa walimpuuza.Msemaji mmoja wa polisi ameahidi kutupa jibu baadaye.

Katika hospitali ya umma, kaunti ya Malindi, ambako tayari chumba cha kuhifadhia maiti kimejaa, familia wamekusanyika wakitaka kujua iwapo jamaa zao ni miongoni mwa maiti zilizo patikana.

Tineja Kijana Issa Ali alipelekwa msitu wa Shakola mwaka wa 2020 na mama yake na ameambia AFP kuwa alipigwa Nthenge alipojaribu kuondoka, lakini baba yake alikuja kumuokoa.

"Mwisho kumuona mama yangu ni mwezi Februari,” aliongeza kijana huyo wa miaka 16.

"Alikuwa hoi sana nilipomuona."

Afisa wa shirika la Red Cross Hassan Musa, aliambia AFP kuwa watu 311 wakiwemo watoto 150 wameripotiwa kutoweka katika mji wa Malindi.

"Tunazungumzia zaidi raia wa Kenya japo kunao Watanzania na wengine kutoka Nigeria. Baadhi yao wametoweka kwa miaka."

Kuongezeka kwa makanisa ya itikadi kama hizi kumesababisha jambo la kutia wasiwasi huku baadhi ya viongozi wao wakitoa mafunzo potofu inayotishia maisha ya waumini wao.

Wengi wa waathiriwa ni watoto

"Hatujui ni makaburi mangapi zaidi bado tutafukua, au maiti ngapi tutakuta” waziri wa masuala ya ndani Kithure Kindiki aliwaambia wanahabari alipozuru eneo hilo siku ya Jumanne akiongeza kuwa uhalifu huo mkubwa kutosha kufunguliwa mashtaka ya kigaidi dhidi ya Nthenge.

Wengi waliofariki ni watoto, kwa mujibu wa duru za kuaminika, kubainisha ukatili wa waumini wa kanisa hilo uliowahimiza wazazi kuwaangamiza wanao.

Hussein Khalid, mkurugenzi mkuu wa shirika la Haki Africa, ambalo ndilo liliwadokezea polisi shughuli za Nthenge an kanisa lake, ameambia AFP kanisa hilo la Good News International linaonekana kuwataka watoto wafe mwanzo, wakifuatiwana wanawake kisha wanaume.

Alisema kuwa asili mia 50 hadi 60 ya waliouawa ni watoto, ambao maiti zao zilikutwa zimefungwa kwa mashuka na kuzikwa katika masimo madogo madogo.

Manabii wa uongo

Rais wa Kenya William Ruto ameazimia kuchukua hatua dhidi ya manabii wa uongo lama vile Nthenge “wanaolenga kutumia kisingizio cha dini kendeleza itikadi potofu zisizokubalika”

Huku uchunguzi ukiendelea, masuali yameibuka ni vipi kanis akama hilo liliweza kuendeleza shughuli zake bila kuugnduliwa licha ya kuwa Nthenge alikuwa tayariu anachunguzwa na polisi tangu miaka sita iliyopita.

Nabii huyo wa televisheni aliwahi kutia nguvuni mwaka wa 2017 kwa shtaka la kuendeleza itikadi kali kufuati agizo lake kwa familia kuwa wasiwapeleke wanao shuleni, akiwashawishi kuwa elimu hiyo haitambuliwi katika bibilia.

Nthenge alikamatwa tena mwezi uliopita, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya baada ya watoto wawili kuuawa kwa kunyimwa kul ana kunywa, chini ya ulinzi ya wazazi wao.

Anatarajiwa kufika mahakamani tarehe 2 mwezi Mei.

TRT Afrika na mashirika ya habari