Benki ya Dunia imetangaza kuwa Uganda kupitisha sheria dhidi ya ushoga haimabatani na matarajio yake  / Picha: Reuters

Rais Yoweri Museveni amesema Uganda itaendelea hata bila msaada wa mikopo kutoka benki ya Dunia.

"Benki ya Dunia na wahusika wengine wanathubutu kutaka kutulazimisha kuacha imani, utamaduni, kanuni na uhuru wetu kwa kutumia pesa. Kwa kweli wanadharau Waafrika wote," rais Museveni amesema katika barua ambayo ameandika na kuweka katika mitandao ya kijamii.

Benki ya Dunia imetangaza kuwa Uganda kupitisha sheria dhidi ya ushoga haiambatani na maadili ya benki hiyo.

"Sheria ya Kupinga Ushoga ya Uganda kimsingi haiambatani na maadili ya Kundi la Benki ya Dunia, " ilisema katika taarifa, "Kujumuika na kutobaguliwa ndio msingi wa kazi yetu kote ulimwenguni."

Rais Museveni amesema tayari sekta binafsi nchini imemea kw akiwango cha kuboresha uchumi.

"Hatuhitaji shinikizo kutoka kwa mtu yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo katika jamii yetu. hayo ni matatizo yetu, " aliongezea.

Rais Museveni amesema uzalishaji wa mafuta ambayo unalengwa kuanza mwaka 2025 itakuwa chanzo kubwa cha mapato ya nchi.

Amesema wataendelea kuzungumza na Benki ya Dunia ili "tuepuke upotoshaji huu ikiwezekana."

Uganda ilipitisha sheria dhidi ya Ushoga mwezi mei mwaka huu.

TRT Afrika