Mbuzi 409 kati ya 850 waliosambazwa kwa wakulima walikufa ndani ya wiki ya kwanza Picha : AP

Bunge limehoji kuhusu Sh7.4M ( dola 2000 ) & Shs400,000 ( dola 109) zilizotumiwa na Wizara ya Kilimo katika ununuzi wa kila mbuzi wa kigeni na wa kienyeji mtawalia,

Mbuzi 409 kati ya 850 waliosambazwa kwa wakulima walikufa ndani ya wiki ya kwanza .

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, Muwanga Kivumbi, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu matokeo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ambapo wabunge walikosoa gharama kubwa zinazotozwa kuwatibu mbuzi hao wagonjwa.

"Wizara ya Kilimo ilihitaji kufanya uangalizi ipasavyo ili kubaini viwango vya kubadilika vya wanyama kwa kuzingatia maeneo ambayo walipaswa kusambazwa. Uchunguzi wa magonjwa uliofanywa baada ya mbuzi hao kuambukizwa ulikuwa zoezi lililochelewa sana,” alisema Muwanga.

Mkaguzi wa serikali alibaini kiwango cha juu sana cha vifo vya mbuzi waliosambazwa chini ya mradi huo.

Kwa mfano, katika wilaya ya Nakasongola, mbuzi wote 150 waliogawiwa wenye thamani ya Sh52.5Mn ( zaidi ya dola 14,149 ) wamekufa, ambapo katika wilaya ya Gomba, kati ya mbuzi 700 waliogawiwa wenye thamani ya Sh245Mn (zaidi ya dola 66,600.

Mbuzi 259 ambao ni asilimia 37 na wenye thamani ya Sh 90.7Milioni ( dola 24,680) walikuwa wamekufa.

Hivyo jumla ya mbuzi 409 kati ya 850 waliosambazwa katika maeneo ya Gomba na Nakasongola wakiwakilisha 45%, wenye thamani ya Sh143 Mn( dola 38,912 walikuwa wamekufa wakati wa ukaguzi Septemba 2023.

"Bei ya wastani kwa kila mbuzi ilitiwa chumvi kwa maoni ya Kamati. Kamati pia inaeleza kutoridhishwa na uwezo wa Sembuguta Estates, Kampuni iliyopewa kandarasi ya kuwasilisha mbuzi hao. Hapo awali ilikuwa imefanya vibaya katika kusimamia miradi kama hiyo. Sembuguta Estates Ltd inapaswa kuorodheshwa kwa kusababisha hasara ya kifedha," Muwanga ameongezea.

Ameomba bunge kutoa angalau miezi 2 kwa Kamati kuchunguza mradi wa mbuzi chini ya wizara ya kilimo.

TRT Afrika