Uzalishaji wa kahawa barani Afrika unapungua kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi. / Picha: Reuters

Viongozi wa Umoja wa Afrika katika mkutano wao kwa kila mwaka tarehe 17 na 18 Februari mwaka huu walikubaliana kwa pamoja kuwa kahawa iangaliwe kama zao la kimkati barani Afrika.

"Huu ni ushindi mkubwa kwa Uganda," Waziri wa Kilimo Frank Tumwebaze amesema katika mtandao wa X.

Uganda ni kati ya wazalishaji wakubwa wa kahawa barani Afrika.

Kulingana na Shirika la Kimataifa la Kahawa, uzalishaji wa kahawa barani Afrika ulipungua kwa asilimia 7.2 kwa mwaka 2022/23 hadi magunia milioni 17.9, kutoka Magunia milioni 19.3 katika mwaka uliopita wa kahawa.

Shirika hilo linasema hii ilifanyika huku sehemu ya soko ya pato la dunia ikishuka kidogo hadi 10.6% kutoka 11.5%.

"Uganda ilikumbwa na upungufu wa uzalishaji kutoka asilimia 6.8 katika mwaka wa kahawa 2022/23 hadi magunia milioni 5.6 kutoka milioni 6.0 mifuko katika mwaka wa kahawa 2021/22.

"Huo ulikuwa ni mwaka wa pili mfululizo wa kushuka kwa uzalishaji, kupungua kwa sababu sawa na ilivyokuwa mwaka wa kahawa 2021/22 yaani kuendelea kwa ukame. Iliripotiwa mara ya kwanza mapema Februari 2022, ukame huu uliathiri maeneo mengi yanayolima kahawa," imesema.

Kwa jumla kuna nchi 25 Barani zinazo wekeza katika uzalishaji wa kahawa.

Ethiopia inaongoza katika uzalishaji wa kahawa lakini nayo pia imekumbwa na athari ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imefanya takriban familia za wakulima wadogo milioni 2.2 zinazojishughulisha na uzalishaji wa kahawa zimepata mapato duni.

Ukame huu pia ulikumba nchi ya Kenya na kupunguza uzalishaji yake.

Kenya ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa kahawa aina ya Arabica barani Afrika, na pato lake lilipungua kwa asili mia 4.6% hadi magunia milioni 0.73 mwaka wa kahawa 2022/23 kutoka magunia milioni 0.76.

Kwa kuiangalia kahawa kama zao la kimkakati inamaanisha kuwa Umoja wa Afrika utaipa kipaombele uzalishaji wa kahawa, na huenda ikaongeza uwekezaji wa kibara wa teknolojia ya kuongeza thamani ya kahawa.

TRT Afrika