Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumamosi alisema kuwa Marekani ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya mpangaji mkuu wa kundi la kigaidi la Daesh na wapiganaji wengine nchini Somalia.
"Leo asubuhi niliamuru mashambulizi ya anga ya Kijeshi dhidi ya Mpangaji Mashambulizi Mkuu wa ISIS [Daesh] na magaidi wengine aliowasajili na kuwaongoza Somalia," Trump alisema kupitia mtandao wa X.
Alisema gaidi huyo alikuwa amejificha kwenye pango na amekuwa akitishia Marekani na washirika wake.
"Mashambulizi hayo yaliharibu mapango wanayoishi, na kuua magaidi wengi bila kwa njia yoyote kuwadhuru raia," alisema.
"Jeshi letu limelenga ,pangaji wa mashambulizi ya ISIS kwa miaka mingi, lakini Biden na wasaidizi wake hawakuchukua hatua ya kutosha kukamilisha kazi hiyo. Mimi nimeifanya!"
Alisema ujumbe kwa Daesh na wengine wote ambao wangeshambulia Wamarekani ni kwamba: "'TUTAKUPATA, NA TUTAKUUA!'"