Mamlaka ya Zambia imewafungulia mashtaka washukiwa watatu wanaotuhumiwa kwa madai ya kuchapisha matamshi ya uchochezi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu afya ya Rais Hakainde Hichilema.
Watatu hao walishtakiwa kwa makosa chini ya sheria za usalama wa mtandao kuhusu unyanyasaji wa kutumia njia za mawasiliano ya kielektroniki, polisi walisema Ijumaa.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambapo machapisho hayo yalichapishwa.
"Wananchi wanaonywa kuhusu kusambaza kwa taarifa za uongo na zenye madhara kwenye majukwaa ya kidijitali kunaweza kusababisha hofu, machafuko na athari za kisheria," msemaji wa polisi Rae Hamoonga aliwaambia waandishi wa habari.
Washukiwa hao wanazuiliwa chini ya ulinzi wa polisi katika eneo lisilojulikana na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Polisi wameonya umma dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kueneza uongo, kuchochea ghasia na kusambaza kashfa.
Wiki iliyopita chama tawala cha UNPD kilisema kuwa rais alikuwa "mwenye afya nzuri na anatekeleza majukumu yake ya kikatiba", katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii waFacebook.
"Puuzeni uvumi wowote kwenye mitandao ya kijamii unaodai vinginevyo," taarifa iliongeza.
Dhamira ya uwazi
Rais Hichilema siku ya Ijumaa alimkaribisha Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughlukia masuala ya Uhuru wa Kujieleza, Irene Khan.
Alisema serikali yake imedhamiria kuendeleza uwazi na mazungumzo yenye tija kwa manufaa ya raia wote, amesema haya kupitia chapisho kwenye jukwaa la X.
Rais huyo anahudumu muhula wake wa kwanza baada ya kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 2021. Alimshinda aliyekuwa rais wakati huo, Rais Edgar Lungu.