Uturiki hadi sasa imetuma misaada muhimu Gaza, kama vile vyakula na dawa. / Picha: AA

Uturuki imesimamisha uuzaji na uagizaji wa bidhaa zote zinazoingia na kutoka Israeli, kama hatua ya adhabu dhidi ya vita vya kikatili vya Tel Aviv dhidi ya Gaza ambavyo vimeua zaidi ya Wapalestina 34,596 katika kipindi cha miezi sita tu.

"Hadi serikali ya Israeli itakaporuhusu uingizaji wa misaada ya kibinadamu Gaza bila ya kizuizi, Uturuki itatekeleza kwa uthabiti hatua hizi mpya hatua mpya ," wizara ya biashara ya Uturuki ilitangaza.

"Awamu ya pili ya hatua ya serikali imetekelezwa, na shughuli zote za usafirishaji na uagizaji bidhaa na Israeli zimesitishwa, zikijumuisha bidhaa zote," iliongeza.

Ankara mwezi uliopita iliweka vikwazo vya kibiashara kwa Israeli, ikieleza kuwa uamuzi huo utaendelea kuwepo hadi Israeli itakapotangaza kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu uingizaji wa kutosha na usioingiliwa wa misaada ya kibinadamu Gaza.

Hapo awali Uturuki ilizuia usafirishaji wa bidhaa aina 54

Aina kadhaa za bidhaa za alumini na chuma, rangi, nyaya za umeme, vifaa vya ujenzi, mafuta na vifaa vingine vilizuiwa tarehe 9 Aprili na wizara ya biashara ya Uturuki.

Uturuki imekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israeli tangu ilipoanzisha kampeni ya kijeshi tarehe 7 Oktoba, huku ikitoa msaada mkubwa wa kibinadamu Gaza tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel, ikiwa ni pamoja na chakula, vifaa vya matibabu, na kuwahamisha maelfu ya wagonjwa.

Zaidi ya Wapalestina 34,500 wameuawa na 77,700 kujeruhiwa katika hujuma ya kikatili ya Israeli huko Gaza, tangu operesheni ya Oktoba 7 ya kundi la Hamas la Palestina dhidi ya Israeli.

Israeli imeweka vizuizi vya kulemaza huko Gaza, na kuwaacha wakazi wake, haswa wakaazi wa kaskazini mwa Gaza, kwenye hatihati ya njaa.

Kulingana na shirika la UN, zaidi ya miezi sita baada ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yalikuwa magofu, na kusukuma asilimia 85 ya wakazi wa eneo hilo kuwa wakimbizi wa ndani huku kukiwa na upungufu wa chakula, maji safi na dawa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo imeiamuru Tel Aviv kuhakikisha vikosi vyake havifanyi mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia huko Gaza.

TRT World