Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika siku ya Jumanne, Erdogan alisisitizia haja ya kuimarisha uhusiano na mshikamano wa nchi hizo mbili./Picha: AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Serbia Aleksandar Vuci, wakigusia mazungumzo ya nchi mbilil, utulivu wa kikanda, na masuala ya ulimwengu, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika siku ya Jumanne, Erdogan alisisitizia haja ya kuimarisha uhusiano na mshikamano wa nchi hizo mbili.

Alionesha matumaini ya Ankara ya uanzishwaji wa haraka wa serikali mpya huko Serbia na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu katika kanda.

Kulingana na Rais Uturuki, nchi yake iko tayari kuimarisha ushirikiano na serikali mpya ya Serbia, pindi itakapoanzishwa.

Ushirikiano wa kiulinzi na kiuchumi

Viongozi hao pia walijadaliana namna ya kukuza ushirikiano wa nchi zao, hususani katika nyanja za kiulinzi. Erdogan alianisha kuwa jitihada za kukuza ushirikiano huu utazaa matunda katika siku zijazo.

Salamu za heri

Erdogan alitumia nafasi hiyo kumtakia nafuu ya haraka Vucic kufuatia ajali ya gari aliyoipata Februari 8.

Kwa upande wake, Vucic alimpongeza Erdogan katika kumbukizi yake ya kuzaliwa.

Mazungumzo hayo ya simu yaliashiria ukuzaji wa uhusiano kati ya Uturuki na Serbia kwa utulivu kwa kikanda.

TRT Afrika