Serikali ya Uturuki iliingilia kati suala hilo kwa haraka, na kutoa sahihisho kwa chombo hicho cha habari kinachomilikiwa na serikali ya Uingereza./Picha: TRT World   

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki imeipinga vikali taarifa ya BBC iliyorushwa siku ya Jumatano ikiwa na kichwa cha habari "Bado tuko vitani... Wakurdi wa Syria wapambana na Uturuki baada ya kuangushwa kwa Assad."

Kulingana na kurugenzi hiyo, madai yaliyochapishwa kwenye taarifa hayo hayana ukweli, yakiwa yameegemea upande mmoja na hayatoi ukweli halisi wa kinachofanywa na Uturuki dhidi ya magaidi kaskazini mwa Syria.

Serikali ya Uturuki iliingilia kati suala hilo kwa haraka, na kutoa sahihisho kwa chombo hicho cha habari kinachomilikiwa na serikali ya Uingereza.

Katika majibu yake, Uturuki ilisisitiza kuwa operesheni zake za kijeshi nchini Syria zinawalenga magaidi wa PKK/YPG na Daesh, na sio raia.

"Uturuki inalenga kupambana na magaidi wanaohatarisha amani ya kanda. Nchi yetu haijihusishi na migogoro yoyote wala kulenga raia," ilisomeka taarifa hiyo.

'Operesheni dhidi ya ugaidi, na si dhidi ya raia'

Uturuki imekuwa mstari wa mbele kuleta utulivu katika eneo la kaskazini mwa Syria toka kwa kuanza kwa machafuko.

Jeshi la Uturuki limeendesha operesheni za kuvuka mipaka kwa kuzingatia sheria za kimataifa, kwa lengo la kulinda mipaka na kuwahakikishia raia wa Syria usalama wao.

Kurugenzi hiyo ya Mawasiliano, ililaani taarifa potofu ya BBC, kwa kutoa taswira mbaya kuhusu Uturuki.

"Ripoti ya BBC inajaribu ktua taswira potofu kwamba Uturuki inaendesha mapambano dhidi ya Wakurdi nchini Syria. Uturuki inaheshimu utawala wa Syria na kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono utulivu wa watu wake," ilisema taarifa hiyo.

"Tofauti na PKK na YPG, ambavyo vina rekodi ya kuendesha uhalifu dhidi ya jamii fulani, Uturuki imeendelea kutoa kipaumbele kwa raia wakati wa operesheni zake,"

Kama ushahidi wa nia yake ya kusimamia tunu za kibinadamu, Uturuki imeendelea kutoa hifadhi kwa mamilioni ya Wasyria, wakiwemo maelfu ya Wakurdi waliokimbia mateso chini ya utawala wa Assad.

Tishio la PKK/YPG kwa utulivu wa Syria

Hali kadhalika, Uturuki ilitoa onyo dhidi ya mashirika ya kigaidi ya PKK/YPG kama tishio la kwa utawala mpya wa Syria.

"Taasisi hizo zinagandamiza umoja wa Syria, kuchochea mgawanyiko wa kijamii huku zikilenga dola haramu kupitia machafuko.

Mara kwa mara, Uturuki imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzitambua PKK/YPG kama tishio kwa amani.

Ankara pia imetoa ushahidi wa hilo.

Mapambano ya Uturuki dhidi ya Daesh

Ankara pia imesisitiza nafasi yake katika mapambano ya kimataifa dhidi ya Daesh na kubainisha kuwa, operesheni zake za kijeshi nchini Syria zinawiana na malengo ya muungano wa kimataifa dhidi ya ugaidi.

"Uturuki imekuwa moja ya nchi zenye ufanisi mkubwa katika vita dhidi ya Daesh, kuwatenganisha makumi ya maelfu ya magaidi na kufanya eneo hilo kuwa salama," ilisema taarifa hiyo.

"Pia tumetoa ulinzi kwa maelfu ya raia wanaokimbia ghasia za Daesh na tumeunga mkono juhudi za kibinadamu za kujenga upya maeneo yaliyoathiriwa."

Kwa kuzingatia juhudi kubwa za Türkiye za kukabiliana na ugaidi, Ankara ilikosoa BBC kwa kuchapisha kile ilichokiita "maudhui ya kupotosha na yenye upendeleo".

"Tunatarajia BBC ichukue mtazamo wa uandishi wa habari wenye malengo na nyanja nyingi badala ya kusambaza taarifa za upande mmoja na zisizo sahihi," ilihitimisha taarifa hiyo.

TRT Afrika