Rais Erdogan Jumanne pia atahudhuria Mkutano wa 44 wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekaribishwa rasmi baada ya kuwasili katika Ikulu ya Lusail mjini Doha, akilakiwa na kiongozi wa taifa hilo Emir Tamim bin Hamad Al Thani.

Erdogan na Al Thani siku ya Jumatatu walijadiliana kuhusu mashambulizi ya Israel huko Gaza.

"Wakati wa mkutano huo, matukio ya hivi punde katika mauaji ya Gaza ya Israel, juhudi za kusitisha mapigano na amani ya kudumu, na hatua zilizochukuliwa na kuchukuliwa ili kupeleka misaada ya kibinadamu Gaza zilijadiliwa," ilisema taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Erdogan alisisitiza kuwa "Israel lazima iwajibike kwa uhalifu wa kivita iliofanya," na kusisitiza umuhimu wa uungwaji mkono wa kimataifa pamoja na juhudi za kisheria kuitaka Israel iwajibike.

Erdogan pia aliahidi kwamba juhudi za Uturuki zitaendelea kuongezeka ili kuhakikisha uwasilishaji wa kutosha wa misaada ya kibinadamu huko Gaza.

"Wakati wa mkutano huo, uhusiano wa Uturuki-Qatar, masuala ya kikanda na kimataifa pia yalitathminiwa," taarifa hiyo ilihitimisha.

Hapo awali, Uturuki na Qatar zilitia saini mikataba 12 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali na tamko la pamoja la mkutano wa 9 wa Kamati Kuu ya Kimkakati ya Uturuki-Qatar.

Erdogan Jumanne pia atahudhuria Mkutano wa 44 wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba.

TRT World