Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema kuwa hakuna shaka kwamba wale waliotekeleza mauaji ya halaiki huko Gaza hatimaye watawajibishwa.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa D-8 mjini Istanbul siku ya Jumamosi, Fidan alisema wale wanaounga mkono amani ya Palestina watashinda.
Mkutano huo uliandaliwa na Uturuki katika Ikulu ya Dolmabahce mjini Istanbul ili kujadili hali ya Gaza.
Jumuiya hiyo inaleta pamoja nchi mbalimbali kutoka mabara matatu, jumla ya watu bilioni 1.2 na pato la taifa kwa jumla la hadi dola trilioni 5, Fidan alisema.
"Leo, kama nchi za D-8, Bangladesh, Misri, Indonesia, Iran, Malaysia, Nigeria, Pakistan na Uturuki, tunatangaza msaada wetu mkubwa kwa Palestina kutoka Istanbul."
Akiangazia kwamba jumuiya hili ina msingi wa kanuni sita - amani, mazungumzo, ushirikiano, haki, usawa na demokrasia, Fidan alisema kwamba kanuni hizi zinafaa zaidi huku ulimwengu unapokabiliana na changamoto na mashaka mbalimbali.
Mkutano huu uliandaliwa ili kuonyesha uungaji mkono zaidi na mshikamano kwa Palestina, aliongeza.
"Zaidi ya hapo awali, Gaza inahitaji matumaini na usaidizi, lakini juu ya yote, inahitaji kuchukuliwa kwa hatua. Vita hivi si vita vya Israeli na Palestina tena bali ni changamoto kwa demokrasia ya kimataifa."
Fidan alisema mfumo wa kimataifa unaporomoka kutokana na "unafiki" wake na "upofu" wa baadhi ya nchi.
'Mmomonyoko wa kanuni na maadili'
Matukio ya Gaza mbele ya macho yao kwa miezi minane iliyopita yanaonyesha mmomonyoko wa kanuni na maadili tangu Oktoba mwaka jana, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alisema.
"Kuendelea kwa mauaji ya Israeli kunachochea jamii na kuwasababishia hasiria zaidi".
“Ikizingatiwa kuwa mfumo wa kimataifa unashindwa kuleta suluhu, ni juu yetu sisi ulimwengu wa Kiislamu kumiliki tatizo hilo na kuongoza kwa suluhu la kudumu,” alisema.
Uturuki inaamini katika kutatua matatizo ya kikanda kupitia suluhu za kikanda, Fidan alisema.
Fidan amesisitiza kuwa tangu siku za mwanzo za vita Jumuiya ya Ushirikiano wa Mataifa ya Kiislamu (OIC) imechukua hatua madhubuti na kwa mara ya kwanza ulimwengu wa Kiislamu umeonyesha misimamo hiyo iliyotatuliwa katika matatizo yake ya kieneo.
"Kuna nchi zinazobadilisha sera zao na nchi zingine kukubali haki ya Palestina."
"Mbali na OIC, juhudi za ulimwengu wa Kiislamu zinaendelea chini ya vikao tofauti kama vile Jumuiya ya Waarabu, Jumuiya ya Nchi za Uturuki na Baraza la Ushirikiano la Ghuba."
'Aibu kwa ubinidamu'
Akieleza kuwa Israeli imefanya uhalifu wote wa jinai uliomo kwenye sheria za kimataifa moja baada ya nyingine, Fidan alisema: "Kinachotokea Gaza ni fedheha kwa ubinadamu."
"Kusimama na Gaza dhidi ya dhulma na ukandamizaji kama huo ni jukumu ambalo sote tunapaswa kutimiza kwa jina la ubinadamu."
Aliongeza ya kuwa, haya ni mapambano ya kudumisha utu na dhidi ya uvamizi, unyakuzi na makazi haramu.
"Kama nchi za D-8, tunasimama pamoja na dhamira ya Palestina. Mkutano wetu wa leo ni uthibitisho wa ahadi yetu."
Fidan alisema Uturuki imejitolea kwa uthabiti katika suluhisho la serikali mbili.
"Kuanzishwa kwa taifa huru, lenye mamlaka na linaloendelea la Palestina kulingana na mipaka ya 1967 na sharti ya kutambulika Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake," alisema.
Alibainisha kuwa pamoja na Hispania, Norway, Ireland, na hivi karibuni zaidi Slovenia kuitambua Palestina kama taifa huru, mamia ya nchi zimesimama dhidi ya "ukosefu wa haki wa kihistoria."
"Wakati mmoja, Palestina itakuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa. Tunatoa wito kwa wengine kulitambua Taifa la Palestina."
"Ni wakati muafaka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzingatia wito huu na sio kuwekwa mateka na nchi moja."