Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Sudan, Abdel Fattah al Burhan, wakijadiliana uhusiano wa nchi mbili, pamoja na maendeleo ya kikanda na ulimwengu.
Katika mazungumzo hayo siku ya Ijumaa, Rais Erdogan aligusia jitihada za kidoplomasia za Uturuki za kuimarisha utulivu wa kikanda, akikumbushia nafasi ya Ankara katika kufanikisha maridhiano kati ya Somalia na Ethiopia kupitia mkataba wa Ankara.
Ameelezea makubaliano hayo kama “hatua madhubuti ya kuchangia amani katika kanda," kulingana na taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Uturuki.
Akizungumzia mgogoro unaoendelea kati ya Sudan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki iko tayari kutatua mgogoro huo.
Pia alisisitizia utayari wa Uturuki katika kukuza amani na utulivu wa Sudan, ikilinda utawala wake dhidi ya kuingiliwa na nchi za nje.
Kuunga mkono umoja wa kisiasa wa Syria na utawala wake
Kulingana na Rais Erdogan, raia wa Syria wamefikia hatua muhimu itakayotoa picha halisi ya mustakabali wao, baada ya miaka 13 ya hali mbaya ya kibinadamu.
Alisisitizia utayari wa Uturuki wa kuunga mkono umoja wa kisiasa wa Syria, akiongeza kuwa Uturuki iko tayari kuiunga mkono serikali ya mpito ili ichukue hatua madhubuti za kuwahudumia wananchi wa Syria bila kusababisha matatizo kwa nchi jirani.
Siku ya Novemba 27, vikosi vinavyopinga utawala wa Syria, viliendesha mapambano ya siku 10, na kufanikiwa kutwaa miji kadhaa, kabla ya kuudhibiti mji wa Damascus siku ya Disemba 8.
Harakati hizo zilisababisha kaunguka kwa utawala wa Assad kabla ya kukimbilia nchini Urusi ambako amepewa hifadhi.