Waziri wa Sheria wa Uturuki amempongeza mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan kwa kutafuta vibali vya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi, akielezea hatua hiyo kuwa "ilicheleweshwa lakini ni nzuri."
Kupitia chapisho katika mtandao wa X iliyosambazwa Jumatatu, Yilmaz Tunc aliikosoa Israeli kwa hatua yake huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023, akidai kwamba vitendo hivi vimekiuka sheria za kimataifa na kupuuza haki za kimsingi za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za kuishi, mali, usalama, na uhuru wa dini na dhamiri.
"Ombi la hati ya kukamatwa la mwendesha mashtaka mkuu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant kwa vita na uhalifu dhidi ya binadamu waliofanya ni uamuzi uliocheleweshwa lakini ni mzuri," Tunc alisema.
Ametaka kesi ya maafisa wa Israel waliohusika na kuwalenga watu wasio na hatia ianze upya haraka iwezekanavyo.
Kuhusika kwa uhalifu wa jinai, Netanyahu na Gallant
"Kama Uturuki, daima tutaweka kwenya ajenda yetu dhuluma, mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaofanywa na Israeli inayoikalia Palestina kwa mabavu kwenye, na tutaendelea kusimama pamoja na ndugu zetu wa Palestina katika malengo yao halali," Tunc aliongeza.
Hapo awali, Khan aliomba hati za kukamatwa kwa Netanyahu, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant na viongozi watatu wa kundi la Palestina Hamas, akiwemo mkuu wa ofisi ya kisiasa Ismail Haniyeh.
Katika taarifa yake, Khan alisema ana sababu za kuridhisha za kuamini kwamba Netanyahu na Gallant wanabeba dhima ya jinai kwa "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu" uliofanywa katika eneo la Palestina, haswa katika Gaza iliyozingirwa, kuanzia angalau Oktoba 8 mwaka jana.
Aliongeza kuwa ofisi yake imetuma maombi ya hati za kukamatwa kwa viongozi watatu wa Hamas - Haniya pamoja na Yahya Sinwar na Mohammed Deif, kwa "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu" uliofanywa Israel na Gaza "kuanzia angalau 7 Oktoba 2023."
Israeli imewauwa zaidi ya Wapalestina 35,500 huko Gaza tangu uvamizi wa Oktoba 7 wa Hamas na kuua watu 1,200. Mashambulio hayo ya angani na ardhini yamesababisha eneo la Palestina kuwa vifusi, na kusababisha watu wengi kuhama makwao na uhaba wa mahitaji ya kimsingi.
Pia ilianzisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo mwezi Januari iliiamuru Tel Aviv kuhakikisha kuwa vikosi vyake havifanyi mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko Gaza.