Maelfu ya watu wameandamana nchini Uturuki wakiiunga mkono Palestina, mwaka mmoja toka kuanza kwa machafuko ya Gaza.
Maandamano hayo yalifanyika siku ya Jumapili, katika majimbo zaidi ya 20 nchini Uturuki, kulingana na waandishi wa habari wa Anadolu.
Katika jiji la Istanbul, asasi za kiraia zilionesha mshikamano wao kwa Palestina.
Hali ilikuwa hivyo hivyo huko Ankara, kama ilivyokuwa katika maeneo mengine ya Kirikkale, Nigde, Hakkari, Yalova, Trabzon, Artvin, Bayburt, Erzurum, Kars, Igdir, Erzincan, Ardahan, Sivas, Van, na Bitlis.
Hata majimbo ya Samsun, Cankiri, Amasya, na Sinop, nayo yalipinga mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza.
Katika eneo la kati la Konya, waandamanji walipinga mashambulizi ya Israeli dhidi ya Palestina na Lebanon.
Ikikaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Israeli imeendelea kuishambulia Gaza tangu Oktoba 7, 2023.
Mashambulizi hayo, yaliyodumu kwa mwaka mmoja sasa, yameua watu takribani 41,900, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine zaidi ya 97,000, kulingana na mamlaka za afya.
Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kufuatia vitendo vyake dhidi ya Gaza.