Wapalestina waandamana kumuenzi mwanaharakati wa Uturuki na Marekani Aysenur Ezgi Eygi, mjini Nablus. /Picha: Reuters

Na Ahmet Yusuf Ozdemir

Kila mtu ambaye amefuatilia miaka 76 ya uvamizi wa Israeli dhidi ya Palestina ana kumbukumbu unaohusiana na uvamizi huo.

Kwa maana hiyo, Palestina ilipata mshikamano zaidi wa kimataifa, ambao unajidhihirisha kupitia maandamano yaliyoandaliwa mitaani, ili kujiweka katika kumbukumbu ya pamoja duniani.

Mazungumzo yoyote ya Palestina yanaleta akilini sio tu bendera ya Palestina au vazi la kitamaduni linaloitwa keffiyah, lakini picha halisi za watu au za kutoka kwa tukio.

Ikiwa ni picha ya kitambo, ya mpiganaji wa upinzani wa Palestina Leila Khaled akiwa amevikwa keffiyah kichwani na Kalashnikov mkononi mwake?

Au video ya zamani ya hotuba maarufu ya kiongozi wa Palestina Yasser Arafat katika Umoja wa Mataifa ambapo alitangaza kwa shangwe kubwa, "Leo ninakuja nikiwa na mpango wa kumaliza mgogoro na bunduki ya mpigania uhuru. Usiache mpango wa kumaliza mgogoro utoke kutoka mkononi mwangu. Narudia, usiache mpango wa huu utoke mkononi mwangu.”

Upinzani wa ndani

Kadiri upinzani dhidi ya uvamizi wa Israeli ulivyozidi kuwa mashinani kwa miaka mingi na kugeuka kuwa maandamano ya mitaani, ukawa sehemu ya utamaduni maarufu kupitia picha au video za watoto wakirusha mawe dhidi ya vifaru.

Kwa mfano, wakati wa Intifadha ya Kwanza iliyodumu kwa miaka sita (1987-93), Ramzi Aburadwan mwenye umri wa miaka minane akawa nembo ya upinzani.

Wakati ambapo mjadala kuhusu "baada ya vita vya kishujaa" ulikuwa ukiongezeka, picha za vijana, badala ya watu mashuhuri, zikawa msukumo mpya kwa vizazi vijavyo.

Katika Intifadha ya pili, ambayo pia inajulikana kama Al Aqsa Intifada, hatima ya wavulana wawili, Muhammad al-Durrah na Faris Odeh, ilishtua ulimwengu.

Muhammad na baba yake, Jamal al-Durrah, walikumbwa na mzozo kati ya Israeli na upinzani wa Wapalestina huko Gaza. Baba yake alipokuwa akipiga kelele na kumfunika mwanawe kutokana na tukio hilo, kamera zilionyesha Muhammad mwenye umri wa miaka 12 akiuawa.

Vile vile, Faris mwenye umri wa miaka 14 alipigwa risasi na wanajeshi wa Israeli alipokuwa akirushia mawe kifaru.

Miaka imepita tangu matukio haya, lakini kitabu cheusi cha Israeli kimepanuka zaidi na kuendelea kuchukua maisha ya watu wasio na hatia, kutoka kwa Shireen Abu Akleh mwenye umri wa miaka 51, mwandishi mashuhuri wa Kipalestina, hadi Hind Rajab mwenye umri wa miaka sita, ambaye simu iliyorekodiwa mara ya mwisho ilikuwa simu ya kuhuzunisha ya kuomba usaidizi.

Polisi wa Israeli walishambulia mazishi ya Abu Akleh, na uchunguzi kwenye gari ambalo Hind alichukua ulionyesha kuwa jeshi la Israeli lilifyatua risasi 335.

Kwa bahati mbaya, unyama huo haujaishia hapo na haujawalenga Wapalestina pekee bali pia wale wanaoonyesha mshikamano na Wapalestina.

Raia kutoka sehemu mbalimbali ya dunia walisafiri kusimama bega kwa bega na Wapalestina. Baadhi yao waliathiriwa na uvamizi wa Israeli.

Mfano wa hivi majuzi zaidi ulikuwa raia wa Marekani-Kituruki Aysenur Ezgi Eygi, mwenye umri wa miaka 26. Alikuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mshikamano (ISM), ambayo imekuwa ikifanya kazi huko Palestina tangu 2001.

Wanajeshi wa Israeli walimuua Eygi mnamo Septemba 6 wakati yeye na wenzake walipokuwa wakipinga uvamizi wa Israeli katika Ukingo wa Magharibi. Eygi hakuwa mwanaharakati wa kwanza wa ISM kuuawa na wanajeshi wa Israeli huko Palestina.

Hata hivyo, ISM iligonga vichwa vya habari miaka miwili baada ya kuanzishwa mwaka 2003 wakati tingatinga la kivita la Israeli lilipomuua mwanaharakati wa Marekani Rachel Corrie mwenye umri wa miaka 23 alipokuwa akipinga Israeli kubomolewa nyumba za Wapalestina.

Je, kuna jambo lolote ambalo Israeli hufanya “kwa makusudi”?

Zaidi ya miongo saba ya historia ya ukaliaji wa mabavu na upinzani umejazwa na mifano wa aina hii mifano na hata zaidi.

Hata hivyo, kadiri matukio na habari zinavyobadilika haraka kila siku, itikio la Waisraeli kwa matukio hayo linaweza kusahaulika mara moja.

Hili lilionekana wazi katika matokeo ya mauaji ya Eygi wakati jeshi la Israeli na Rais wa Merika Joe Biden wote walibishana kwamba hii ilikuwa "ajali" na "kuna uwezekano mkubwa kwamba alipigwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na bila kukusudia".

Hili linaweza kuwashangaza wengine, lakini imekuwa sera ya Israeli kumlaumu mwathiriwa kwa kuwa "mahali pabaya kwa wakati usiyo muafaka".

Ili kujipurukusha na suala la ukaliaji wa mabavu wa kimfumo, Israeli inaweka juhudi kubwa katika kukabiliana na madai ya mauji na kuligeuza kuwa suala la mtu mmoja au tukio moja.

Kuuawa kwa Muhammad al-Durrah ni mfano wa kutosha wa kuchambuliwa kwa kina.

Baada ya kukubali jukumu la kuhusika kwa mauaji hapo awali, baadaye Israeli ilidai y al Durrah aliuawa kutumia risasi zilizofyatuliwa na Wapalestina. Mbaya zaidi waliendela kudai kwamba tukio hilo lilipangwa na wapiganaji wa Kipalestina, mpiga picha, na babake Muhammad.

Kwa upande wa Rachel Corrie, mtindo kama huu ulitumika

Msemaji wa jeshi la Israeli alielezea wanaharakati wa ISM ya kuwa "kundi la waandamanaji ambao walikuwa hawakuajibika, wakiweka kila mtu katika hatari - wakiwemo Wapalestina, wao wenyewe, na vikosi vyetu - kwa kujiweka kwa makusudi katika eneo la mapigano."

Hata ingawa tingatinga lilimgonga Corrie, dereva alidai kwamba hakuweza kuona hilo.

Hatimaye, hakimu katika mahakama ya Israeli, akijibu kesi iliyowasilishwa na familia ya Corrie, aliamua kwamba kifo chake kilikuwa "matokeo ya ajali aliyojitakia".

Wakati wa mauaji ya kimbari, Israeli inatumia mfumo huo.

Shambulio hilo lililotokea tarehe 17 Oktoba katika Hospitali ya Al Ahli Arab lilikuwa tukio muhimu katika suala hilo.

Badala ya kuruhusu uchunguzi wa kimataifa kufanyikai, Israeli na, mara hii, washirika wake walikimbilia kuthibitisha kwamba chanzo cha "mlipuko" sio Israeli bali Wapalestina kwa kuchambua picha kutoka eneo la tukio.

Israel inataka wale wanaofuatilia matukio kuamini hadithi zinazosimuliwa na upande wa Israeli, ambapo madai ya Wapalestina ni "uzushi" tu.

Hii inaacha nyuma maswali mengi, bila shaka, kama vile ukosoaji na uhalifu gani unastahili kuchunguzwa au kama kuna uhalifu wowote ambao Israeli inatenda kwa makusudi.

Mwandishi, Ahmet Yusuf Ozdemir ni Profesa Msaidizi wa Sayansi ya Siasa na Idara ya Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ibn Haldun.

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT World