Uturuki na Italia wameomba kuandaa kwa pamoja Mashindano ya kandanda ya Ulaya 2032 huku wakiwa wawaniaji pekee, UEFA ilisema.
Mashirikisho hayo mawili ya soka yamekuwa yakigombea katika zabuni ambayo ilipangiwa kupigiwa kura Oktoba 10 na wajumbe wa kamati kuu ya UEFA.
Uamuzi wao wa kuungana kwa pamoja unawahakikishia wale waliopewa nafasi kubwa ya kuandaa Euro 2028 ambayo ni mashirikisho manne ya Uingereza na Ireland kushinda zabuni kama inavyotarajiwa siku hiyo hiyo.
"Itakuwa hatua muhimu kwa Uturuki, Iwapo UEFA itakubali ombi letu la pamoja la EURO 2032, tutajiondoa kwenye EURO 2028," Rais wa Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) Mehmet Buyukeksi alisema Ijumaa.
Aidha, Kuungana kutapunguza hatari ya UEFA ya kumteua mwenyeji pekee, zikiwa tu zimesalia miaka tisa kabla ya mashindano ya timu 24, na michezo 51 ambayo huenda yakahitaji kutumia viwanja 10 mnamo Juni na Julai.
Iwapo UEFA itakosa kuridhia ombi la Uturuki, itaenda kinyume na ahadi yake ya kufikia kiwango cha sifuri cha kaboni katika matukio yake ifikapo 2040, kwani Italia italazimika kujenga viwanja vipya na Roma na Istanbul zikitenganishwa kwa takriban kilomita 1,400 tu huku safari za ndege zikichukua zaidi ya saa mbili.
Mahitaji ya miundombinu
Italia inahitaji kujenga na kukarabati baadhi ya viwanja vya zamani .
Miradi ya ujenzi nchini Italia, kama vile kukarabati uwanja wa San Siro huko Milan, inaweza kuwa ya urasimu na polepole.
Roma ililenga kuwa na uwanja mpya wazi kwa msimu wa 2016-17 lakini bado iko katika Stadio Olimpico ambayo ilitumika kwa michezo ya Euro 2020.
Uturuki ina viwanja na miundombinu karibu tayari kabisa baada ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kitaifa chini ya miongo miwili ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdogan.
Kuandaa kwa pamoja bila kura za ushindani kutakuwa suluhu la kimaadili kwa Uturuki baada ya zabuni kadhaa kushindwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na maswali mapya kuhusu uwezo wake wa kuandaa baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Istanbul mwezi uliopita.
Mashabiki wa Manchester City na hata maafisa wakuu wa UEFA ambao watachagua mwenyeji wa 2032, walikabiliwa na changamoto za vifaa jijini na karibu na Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk wenye uwezo wa kuwalaki watu 72,000.
UEFA imesema sasa itafanya kazi na mashirikisho hayo mawili ili kuhakikisha zabuni yao ya pamoja inakidhi mahitaji yote ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu 24.
Shirikisho la soka Uturuki lilisema katika taarifa yake, Euro 2032 "itagawanywa kwa usawa kati ya nchi hizo mbili" bila maamuzi bado ni miji gani na viwanja vitachaguliwa.
Ingawa Uturuki pia inawania kuandaa toleo la 2028, ambalo limepangwa kwa muda mrefu kwa Uingereza na Ireland tangu walipojiondoa kwa idhini ya UEFA kutoka kwa shindano la Kombe la Dunia la 2030.
UEFA inataka ombi moja pekee la Uropa kwa Kombe hilo la Dunia na mgombea anayependelewa ni ofa ya Uhispania na Ureno ambayo sasa inajumuisha Morocco na Ukraine. Kura ya FIFA imepangwa mwishoni mwa 2024.
Shirikisho la UEFA linapaswa kufanya uteuzi wa kuandaa Euro zote mbili ifikapo Oktoba 10 katika makao makuu yake huko Nyon, Uswizi.