Ligi kuu ya soka nchini Uturuki imeshuhudia uhamisho wa jumla ya wachezaji 276 kwa vilabu 20 kuu vya ligi hiyo wakiwemo ni pamoja na wachezaji 85 kutoka ndani ya Uturuki na 191 waliojiunga na timu hizo kutoka nje ya nchi katika dirisha la uhamisho wa ligi lililoanza Juni 26 na kudumu siku 82.
Dirisha dogo la uhamisho na usajili wa pili maarufu "uhamisho wa kati" litafunguliwa tena tarehe 11 Januari 2024 na kukamilika tarehe 9 Februari 2024,
Senegal ndio taifa lenye wanasoka wengi waliohamia timu za Super Lig, wachezaji 8 wakiwa wametokea nchi hio.
Wanasoka sita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ivory Coast na Cameroon wamejiunga na timu za Super Lig ya Uturuki.
- Nigeria wachezaji wanne
- Algeria, Guinea na Visiwa vya Cape Verde wachezaji watatu
- Mali, Morocco, Kongo, na Misri Wachezaji wawili
- Mataifa yanayowakilishwa na mchezaji mmoja pekee ni Guinea-Bissau, Ghana, Gambia, Gabon, Angola, na Chad
Baadhi ya vilabu vikuu vimewasajili wachezaji wa bara Afrika ili kuviimarisha vikosi vyao msimu huu.
Galatasaray: Wilfried Zaha, Hakim Ziyech, Cedric Bakambu.
Fenerbahce: Alexander Djiku, Omar Fayed.
Besiktas: Jean Onana, Daniel Amartey, Eric Bailly, Arthur Masuaku.
Trabzonspor: Nicolas Pepe, Batista Mendy, Paul Onuachu.
RAMS Başakşehir: Ousseynou Ba, Jerome Opoku, Mehdi Abeid, Emmanuel Dennis.
Kasımpaşa: Kenneth Omeruo, Driess Saddiki, Julien Ngoy, Samuel Bastien.
İstanbulspor: Alassane Ndao, Mandy Mamadou, David Sambissa,Djakaridja Junior Traoré, Racine Coly.