DIDIER DROGBA
Nyota huyu raia wa Ivory Coast alicheza katika ligi kuu ya Uturuki ‘Super League’ kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya kusajiliwa na klabu ya Galatasaray akitokea Shanghai ya Uchina.
Drogba alicheza jumla ya mechi 53 na kufunga magoli 20 huku akitoa usaidizi katika kufunga (assist) magoli 13.
JAY- JAY OKOCHA
Kiungo huyu wa kati kutoka Nigeria alijiunga na klabu ya Fenerbahce mwaka 1996 akitokea klabu ya Frankfurt.
Okocha aliifungia Fenerbahce magoli 32 katika mechi 76 alizocheza huku akisaidia kufunga magoli 19, kabla ya kusajiliwa na PSG kwa dau la euro milioni 17.
NJITAP GEREMI
Geremi aliichezea klabu ya Genclerbirligi kwa misimu miwili kabla ya kusajiliwa na Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne. Aidha pia aliwahi kuchezea Chelsea na Newscastle kabla ya kurejea tena Uturuki mwaka 2010 kuichezea klabu ya MKE Ankaragucu.
Njitap alifunga jumla ya magoli 11 kwenye mechi 69 alizocheza. Uturuki.
SAMUEL ETO’O
Mshambulaiji huyu raia wa Cameroon ni moja kati ya wachezaji nyota waliowahi kucheza nchini Uturuki..
Baada ya kung’ara ulaya akichezea Barcelona, Inter na Chelsea, Eto’o alitua Uturuki mwaka 2015 kuichezea klabu ya Antalyaspor.
Kabla ya kutangaza kustaafu rasmi mwaka 2020, Eto’o alikuwa pia ameitumikia klabu ya Konyaspor. Nyota huyo alifunga jumla ya magoli 50 nchini Uturuki.
EMMANUEL ADEBAYOR
Baada ya kuchezea klabu kadhaa za Ligi Kuu ya Uingereza zikiwemo Tottenham (kati ya 2012 na 2015) na Crystal Palace (kati ya 2015 na 2017),
Adebayor hatimaye alitua Uturuki mwaka 2017 baada ya kusajiliwa na klabu ya Basaksehir na baada ya hapo akahamia klabu ya Kayserispor.
Mshambuliaji huyo alifunga jumla ya magoli 26 nchini Uturuki.
DEMBA BA
Mshambuliaji huyu raia wa Senegal alijiunga na klabu ya Besiktas mwaka 2014 kabla ya kuelekea China mwaka mmoja baadae. Demba Ba alirejea tena Uturuki na kuchezea klabu ya Goztepe na Basaksehir kabla ya kutangaza kustaafu soka mwaka 2021.
Alifunga jumla ya magoli 46 kwenye mechi 103 alizocheza katika Ligi Kuu ya Uturuki.
(Chanzo – GOAL)