Manchester United sasa wanatazamia kuondoka mapema katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA kufuatia kupoteza kwa Galatasaray siku ya Jumanne. / Picha: Reuters

Mauro Icardi alifunga dakika ya 81 pale Galatasaray ilipoishinda Manchester United 3-2 kwenye Ligi ya klabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne na kuongeza shinikizo kwa meneja Erik ten Hag.

Mshambulizi huyo tayari alikuwa amepoteza nafasi ya mkwaju wa penalti ambayo i ngeiweka timu ya Uturuki mbele katika uwanja wa Old Trafford. Lakini aliweza kujimkomboa kwa ustadi zaidi alipodakia pasi ya kichwa ya Davinson Sanchez kabla ya kuinua shuti lililomshinda kipa wa United Andre Onana.

Kilikuwa ni kipigo cha sita kwa United katika mechi kumi msimu huu na cha pili katika mechi zake mbili za ufunguzi katika Kundi A la Ligi ya Mabingwa.

Na kama kutonesha kidonda kwa Ten Hag , timu yake ilikuwa imeongoza mara mbili kupitia mabao ya Rasmus Hojlund katika kila kipindi.

Majibu ya haraka

Lakini mara zote mbili Galatasaray ilitoa majibu ya haraka kwa matokeo, huku Casemiro akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Dries Mertens kwa mkwaju wa penalti dakika ya 76.

Hojlund aliifungia United bao la kuongoza dakika ya 17 kwa kichwa kutoka kwa shuti kali, lakini bao la kuongoza halikudumu kwa muda mrefu kwani Wilfried Zaha alisawazisha dakika ya 23.

Hojlund alifunga tena dakika ya 67 alipoudaka mpira uliotoka nje kutoka kwa Sergio Oliveira karibu na mstari wa katikati, akasogeza mbele na kumalizia kumpita kipa wa Galatasaray Fernando Muslera.

Wageni walisawazisha tena dakika nne baadaye huku Kerem Akturkoglu akimalizia kazi kutoka ndani ya eneo la goli.

Punde tu baada ya Mertens kuingia eneo la hatari akichukua pasi ya Onana, lakini aliangushwa na Casemiro kabla hajapiga shuti na Mbrazili huyo akaonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Icardi alipiga shuti nje ya mkwaju wa penalti, lakini akaweza kukomboa sura alipofunga bao la ushindi dakika chache baadaye.

Manchester United sasa wanatazamia kuondoka mapema katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA kufuatia kupoteza kwa Galatasaray siku ya Jumanne.

TRT Afrika