Kombe hilo la UEFA Euro 2024 litachezwa kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 nchini Ujerumani / Picha: Reuters

Bingwa mtetezi Italia amepangwa katika kundi moja na Uhispania katika droo ya Euro 2024 iliyofanywa siku ya Jumamosi, huku Ufaransa ikiwekwa kundi moja kuchuana na Uholanzi.

Kombe hilo la Euro 2024 litakalochezwa mwezi mzima, katika miji 10 nchini Ujerumani, litahitimishwa na fainali itakayopigwa mjini Berlin, Ujerumani Julai 14.

Kundi B: Uhispania, Croatia, Italia, na Albania

Italia, ambayo iliicharaza England kwa penalti huko Wembley katika fainali ya makala ya mwisho ya Dimba la Uropa mnamo 2021, pia itakabiliana na Kroatia na Albania katika Kundi B.

Uhispania, mshindi dhidi ya Italia kwenye fainali za Euro 2012, itacheza mechi yao ya ufunguzi mjini Berlin Juni 15 dhidi ya Croatia, iliyomaliza nafasi ya pili Kombe La Dunia 2018.

Kundi D: Uholanzi, Austria, Ufaransa na Mshindi kati ya Poland/Wales/Finland/Estonia

Mechi hiyo kati ya Ufaransa, iliyomaliza ya pili fainali ya Kombe la Dunia 2022, na Uholanzi, itakuwa mechi nyingine ya uzani mzito katika michuano ya ufunguzi huku wawili hao wakiwa kundi D pamoja na Austria na mshindi wa mchuano wa mtoano kati ya Poland, Wales, Finland au Estonia.

Kundi C: Slovenia, Denmark, Serbia, na England

England iliponea kwa kujiepusha na mpinzani yeyote mgumu.

England itakutana na Slovenia, Denmark na Serbia, huku Wenyeji, Ujerumani wakichuana Na Scotland katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo Juni 14, mjini Munich.

Kundi A: Ujerumani, Scotland, Hungary, na Uswizi

Washindi wa Kombe la Euro 2016 Ureno wamejumuishwa Kundi F pamoja na Uturuki, Jamhuri ya Czech na mshindi wa mchuano wa mtoano kati ya Ugiriki, Georgia, Luxemburg au Kazakhstan.

Kundi F: Uturuki, Ureno, Czechia na mshindi kati ya Ugiriki/Georgia/Luxemburg/ Kazakhstan.

Ubelgiji iko Katika kundi E pamoja na Slovakia, Romania mshindi wa mchuano wa mtoano kati ya Israel, Iceland, Bosnia na Herzegovina au Ukraine.

Kundi E: Ubelgiji, Slovakia, Romania, na mshindi kati ya Israel/Iceland/Ukraine/Bosnia na Herzegovina.

Baadaya ya mechi yake ya ufunguzi, Ujerumani itakabiliana na Hungary; wapinzani wao wa fainali ya Kombe la Dunia 1954, watakapokutana huko Stuttgart tarehe 19 Juni, 2024.

Ujerumani itacheza mechi yake ya mwisho ya makundi dhidi ya Uswisi mjini Frankfurt mnamo Juni 23, na nchi hizo mbili jirani hazijawahi kukutana kwenye Euro.

AFP