Klabu ya Arsenal kabla ya mechi yake ya UEFA Champions League. Picha: UEFA

Timu 32 zinazoshiriki hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa UEFA msimu huu wa 2023/24, zitashuka dimbani siku ya Jumanne kuwania ubingwa wa kombe hilo.

Manchester United VS Galatasaray (Old Trafford)

Manchester United itawapokea mababe wa Uturuki, Galatasaray, ugani Old Trafford huku ikisaka kurejesha tabasamu kwa nyuso za mashabiki wa 'The Red Devils' baada ya kulazwa na Bayern 4-3 ugenini kwenye mechi yake ya ufunguzi, UEFA Champions League.

Mechi hiyo itasimamiwa na refa Ivan Kružliak kutoka (Slovakia).

Lens VS Arsenal

Klabu ya Ufaransa ya Lens itakuwa mwenyeji wa Arsenal ambao waliisambaratisha PSV 4-0 uwanjani Emirates katika mchezo wao wa kwanza, mechi za makundi wakati Lens walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Sevilla ya Uhispania. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Marco Guida wa (Italia).

Napoli VS Real Madrid

Real Madrid itachuana na Napoli, mechi ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, katika Uwanja wa Diego Armando Maradona. Baada ya kuchupa hadi juu ya jedwali LaLiga, Real madrid sasa inalenga kuchukua uongozi wa Kundi C, linaloongozwa na Napoli baada ya kuwapiga Union Berlin 1-0 katika mechi yao ya ufunguzi. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Clément Turpin wa (Ufaransa).

PSV Eindhoven VS Sevilla

Waholanzi PSV wanatarajia kusajili matokeo bora wakiwa wenyeji, baada ya kushinda mechi zao tano za mwisho nyumbani katika mashindano ya Uropa, na kufunga mabao 18 katika mchakato huo. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Daniele Orsato wa (Italia).

Ratiba ya Mechi zaidi za siku ya Jumanne.

  • Inter VS Benfica
  • Union Berlin VS Braga
  • Salzburg VS Real Sociedad
  • Copenhagen VS Bayern

Fainali ya Ligi ya Mabingwa UEFA 2023/24 itapigwa katika uwanja wa Kihistoria Wa Wembley, jijini London.

TRT Afrika