Kabla ya kustaafu 2009, Montella alicheza Roma kwa miaka mingi, ambapo alishinda taji la Italia la Serie A, Kombe la Italia na Kombe La Super. Picha: Photo: Reuters Archive

TFF imetangaza kufikia makubaliano ya miaka 3 na mwalimu Vincenzo Montella na kumkabidhi wadhifa wa kuinoa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Uturuki.

Hii ni baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo kukatiza makubaliano na mkufunzi wake wa zamani Stefan Kuntz na kuagana naye.

Montella atakaribishwa rasmi kwenye sherehe ya kusaini mkataba Jumatano, Septemba 27, 2023 katika kambi ya mafunzo ya timu za Taifa TFF Hasan Doğan.

"Tunamtakia Kocha wetu mpya wa Timu ya Taifa, Vincenzo Montella, mafanikio katika kazi yake," TFF Ilisema.

Montella mwenye wasifu wa kuvutia, amewahi kufundisha klabu nyingi kama Roma, Catania, Fiorentina, Sampdoria, AC Milan Nchini Italia, na Sevilla ya Uhispania na klabu ya kituruki Adana Demirspor.

Aliiongoza AC Milan kwenye ushindi wa kombe la Super La italia msimu wa 2016-17.

AA