Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano ya soka kati ya Shule za Afrika 2024. Picha: CAF

Zanzibar, imechaguliwa kuwa mwenyeji la Fainali za Mashindano ya soka kati ya Shule za Afrika, Caf 2024.

Shindano hilo linaloingia katika msimu wake wa pili wa fainali kubwa zaidi za mashindano ya soka kwa vijana barani Afrika, litaandaliwa katika uwanja wa Amani uliokarabatiwa kati ya tarehe 21-24 Mei 2024.

Mashindano ya soka ya shule za Afrika Caf yanawajumuisha wavulana na wasichana chini ya umri wa miaka 15.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na baadhi ya nyota wastaafu watakaosaidia kuhamasisha na kuwapa motisha wanasoka chipukizi.

Washindi wa pande zote, kwa wavulana na wasichana watapokea tuzo ya dola 300,000, mshindi wa medali ya fedha 200,000, nao washindi wa medali ya shaba wakitarajiwa kuondoka na dola 150,000.

TRT Afrika na mashirika ya habari