Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limetangaza ushirikiano wa pamoja wa Uturuki na Italia kuwa wenyeji wa mashindano ya soka bara Ulaya ya 2032 (EURO 2032).
Mkutano wa bodi ya Utekelezaji ya UEFA uliofanyika katika makao makuu ya UEFA, Nyon, ilitangaza kuwa zabuni ya pamoja ya Uturuki na Italia ndio imechaguliwa kuwa wenyeji wa EURO 2032.
Uturuki iliwakilishwa kwenye mkutano huo na Rais wa shirikisho la soka TFF Mehmet Büyükekşi, naibu wake Mustafa Eröğüt, Katibu Mkuu Kadir Kardaş na mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya soka ya Atakaş Hatayspor Volkan Demirel, ambaye ni balozi wa zabuni ya Uturuki EURO 2032.
Hatua ya UEFA inamaanisha kuwa Uturuki, ambayo itaandaa mashindano ya soka ya Ulaya ya 2032 (EURO 2032) kwa Pamoja na Italia, itaweka historia kwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya soka ya mataifa ya Ulaya kwa mara yake ya kwanza.
Mashirikisho ya soka ya Uingereza, Ireland ya Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Scotland na Wales nayo yametunukiwa kuwa wenyeji wa UEFA EURO 2028 baada ya kuwasilisha zabuni ya pamoja.