Kocha mpya wa Uganda Paul Put. Picha: FUFA
Shirikisho la Soka nchini Uganda (FUFA) chini ya rais Magogo Moses Hassim, limetangza kumsajili kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka.

FUFA ilitangazo uteuzi huo mapema alhamisi kwenye mkutano maalum wa waandishi wa habari katika majengo ya FUFA, Mengo.

"Kocha Paul Put alisaidia Burkina Faso kufikia fainali ya kombe la AFCON mwaka 2013, aliiongoza Guinea kufika robo fainali na pia aliiwezesha Gambia kufuzu AFCON. Kwa wasifu kama huu, tunaamini kocha atafanya kazi nzuri hapa." Rais wa FUFA Magogo Moses alisisitiza.

Mniamini, mnipe muda

Kwa upande wake, Kocha Paul Put ameliomba FUFA kumuamini na kumpa muda wa kutosha kufanikisha matokeo mazuri kwa timu hiyo.

"Tafadhali nipe muda, nipe ujasiri. Utaona timu tofauti ya kitaifa."Paul Put alisema

Uganda iko kundi moja na Algeria, Guinea, Msumbiji, Botswana na Somalia katika kundi G kwa minajili ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026, mataifa ya Afrika.

"FUFA iliandaa mchakato wa maombi na tulipata makocha zaidi ya 150 wakiwemo Waganda 2 walioomba kazi hiyo. Baada ya uchambuzi wa kina, Mtendaji w FUFA walimpendekeza Paul Put na tunaamini atafanya kazi nzuri," Rais wa FUFA Magogo amesema.

Kocha huyo mpya wa Uganda Cranes ameajiriwa pamoja na benchi la ufundi Sven De Wilde, Mathieu Denis, Gerry Oster, Martin Michiel, Na Jelle Sevenhant huku rais wa FUFA akisema atasaidiwa na baadhi ya wakufunzi wa Uganda.

"Wakati huu, tumemruhusu kocha kuteua wafanyikazi wake wa nyuma na anakuja na watu wengine watano kutoka Ubelgiji. Hata hivyo, Kutakuwa na Waganda ambao watafanya Kazi kama sehemu ya wafanyakazi benchi la ufundi."Rais wa FUFA aliongeza.

Uteuzi wa Paul Put unajiri baada ya shirikisho la FUFA na kocha wa zamani wa timu ya soka ya Uganda Milutin Sredojevic, kukubaliana kukatiza mkataba wa makubaliano kati ya pande hizo mbili mnamo 14 septemba 2023,.

TRT Afrika